Header Ads Widget

ONYO KALI LATOLEWA KWA WAANDIKISHAJI UCHAGUZI NJOMBE DC KUTUNZA SIRI.

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Serikali wilayani Njombe Mkoani Njombe imewaonya waandikishaji wa vituo 227 vya uchaguzi waliokula kiapo Cha utii na Uadilifu kutotoa siri za mchakato huo kwani ni kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Onyo hilo limetolewa na mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe George Makacha wakati akiwaapisha waandikishaji hao  katika ngazi za vijiji na Kata zoezi lililofanyika Mtwango.


Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi na Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe CPA Asha Msangi Amesema hakuna kumuacha mwananchi yeyote mwenye sifa ya kuandikishwa katika kipindi cha siku kumi. 

Baadhi ya waandikishaji waliokula kiapo na mafunzo ya kwenda kutekeleza zoezi hilo akiwemo Wema Chilonwa na Andrea Mara wanaahidi kwenda kutunza siri za viapo vyao na kwamba watafanyakazi ya kuwaandikisha wananchi kwa kadri ya uwezo wao.


Jumla ya vijiji 45 vya kata 12 za Halmashauri hiyo vinakwenda kushiriki katika zoezi hilo kwa jumla ya vitongoji 227.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI