Na Ashrack Miraji Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, amewashukuru waandaaji wa Shindano la Samia Challenge kwa kuunga mkono juhudi za Serikali na kuchagua kufanyika katika mkoa wa Tanga. Akizungumza katika hafla hiyo, Kubecha alisema mkoa uko tayari kwa matukio mengine ya aina hiyo.
"Kwanza, nimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuweza kutuleta pamoja hapa leo, tukijadili mafanikio yaliyopatikana kupitia Samia Challenge. Tunashuhudia matokeo chanya katika sekta mbalimbali," alisema Kubecha.
Alisisitiza umuhimu wa kuimarisha demokrasia na diplomasia chini ya uongozi wa Rais Samia, akisema, "Ni lazima tumshukuru Rais kwa juhudi zake za kuimarisha makundi mbalimbali, na tunajivunia maendeleo makubwa yanayoendelea nchini."
Aidha, Kubecha alisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kulitaja jina la Rais Dkt. Samia Suluhu kwa sababu ya mafanikio ambayo mkoa wa Tanga na taifa kwa ujumla yameyapata.
"Niwapongeza washindi wa Samia Challenge, ambao walikuwa wanatafutwa watatu kwa ajili ya kuonyesha umahiri wa Rais katika kuleta mabadiliko. Pia, kupitia mikopo ya asilimia 10, tunatakiwa kuangalia namna ya kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kupitia asilimia 2 ya mikopo yao," aliongeza.
Kubecha alihitimisha kwa kusema kwamba juhudi hizi zinahitaji kuungwa mkono ili kuendeleza maendeleo katika wilaya ya Tanga.
0 Comments