Na Elizabeth Ntambala Matukio Daima App
MKUU wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Peter Lijualikali ameongoza wakazi wa wilaya Nkasi Kwa kujiandikisha kwenye daftari la wakazi Kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,mwaka Huu.
Mkuu huyo wa wilaya amejiandikisha kwenye kitongoji chake Cha juhudi kilichopo kata ya Nkomolo wilayani Nkasi.
Akizungumza mara baada ya kujiandikisha amesema kujiandikisha kwenye daftari Hilo litawafanya Wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwenye vitongoji na vijiji vyao.
Alidai kuwa licha ya kujiandikisha Kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Bali pia litatumika kama orodha ya wakazi kwenye kitongoji husika na kuwa hiyo Sasa ni fursa Kwa Kila mmoja kujiandikisha.
Hivyo aliwataka Wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika kitongoji hicho Cha Juhudi kuendelea kuwahamasisha wenzao Kwa kuhakikisha Kila mmoja anajitokeza na kwenda kujiandikisha kwenye kitongoji Ili aweze kupata haki ya kupiga kura ikiwa ni pamoja na jina lake kuwa sehemu ya orodha ya wakazi katika kitongoji husika.
Sambamba na Hilo amesisitiza kuwa uchaguzi huo unatarajia kuwa ni uchaguzi huru na wa haki lakini pia amewataka Wananchi kushiriki kwenye mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua ya awali ya ushawishi Kwa Watu wenye uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
Wananchi wameendelea kujitokeza Kwa wingi Kwa siku ya kwanza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura huku hari ikiwa shwari katika maeneo mbalimbali ya wilaya Nkasi
0 Comments