Na Matukio Daima App
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yameanza Rasmi Leo okctoba 1 /2024 huku Chifu Adam Abdul Mkwawa akiongoza kundi la wazee wa Kihehe kwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Chifu Mkwawa na wasaidizi wake hao wameondoka asubuhi ya leo kwa magari maalum ya utalii kutoka Hifadhi ya Ruaha .
Ziara ya Chifu Mkwawa na wasaidizi wake imeanzia viwanja vya Boma mjini Iringa kwa wazee hao maarufu kwenda kufungua rasmi sehemu ya Maadhimisho kwa kufanya utalii wa ndani na sawa na kufungua milango ili makundi mengine na mtu mmoja mmoja kutumia Siku Hizi saba za Maadhimisho kwenda kutalii.
Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Ruaha yameanza leo Okyoba1-7/2024 yatafungwa na Waziri Balozi Dkt Pindi Chama kwa Kuzindua utalii wa Puto.
Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha, Godwel Ole Meing’ataki alisema maandalizi ya maadhimisho hayo yatatanguliwa na shughuli mbali mbali za kijamii pamoja na elimu juu ya umuhimu wa Hifadhi hiyo.
Alisema kuwa Hifadhi imejipanga kuimarisha uhusiano na jamii mbalimbali, ikiwemo watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuwapatia fursa ya kutembelea hifadhi hiyo pamoja na kutoa msaada kwa familia zenye mazingira magumu
“Nitumie fursa hii kuwakaribisha Watanzania wote, hususan wakazi wa Iringa, katika maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo yameanza leo tarehe 1 hadi 7 Oktoba, 2024, huku kilele chake kikitarajiwa kuwa tarehe saba,” alisema Meing’ataki.
0 Comments