Boniface Jacob akiwa mahakamani
Na matukio daina App,
kada wa chadema Boniface Jacob ameendelea kusota kwenye viunga vya Mahakama ya kusutu kufuatia kukosa dhamana mara baada ya uamuzi mdogo kuhusu dhamana hiyo kutotolewa.
Kesi hiyo iliitwa hii leo tarehe 01 Oktoba 2024 kwa ajili ya kutolewa kwa maamuzi mawili madogo, moja ikiwa kuhusu kiapo cha ziada kilichowasilishwa na upande wa mashtaka na maamuzi mengine yakiwa kuhusu dhamana ya Boni.
kesi hiyo ambayo ipo mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Franco Kiswagwa, alitoa uamuzi mmoja kuhusu kiapo cha ziada ambacho Mahakama hiyo imekikaataa kwa kukubaliana na hoja za upande wa washitakiwa.
Kuhusu uamuzi wa dhamana ya Boni, Mahakama hiyo imesema itautoa tarehe 7 Octoba 2024.
Boni alifikishwa Mahakani hapo kwa mara ya kwanza tarehe 19 Septemba 2024, mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Franco Kiswagwa na kusomewa mashtaka mawili.
Kosa la kwanza linalomkabili Boniface Jacob linahusu kuchapisha taarifa za uongo mnamo tarehe 12 Septemba 2024, ambapo alidai kuwa Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kwa kupotea kwa wanafamilia wa hizo familia.
Kosa la pili, ambalo lilitokea tarehe 14 Septemba 2024, linahusiana na kuchapisha taarifa nyingine za uongo zinazosomeka ‘Polisi wanatesa watu na kuua ndio kazi wanaweza’. Boniface amekana mashtaka yote hayo.
Ikumbukwe hapo awali uamuzi wa kuhusiana na dhamana ya Boni ulitakiwa kutolewa Jumatatu ya tarehe 23 Septemba 2024, lakini ilishindikana kufuatia serikali kutomleta mtuhumiwa Mahakamani kwa madai ya kuwa, magereza walikosa usafiri wa kumleta Mahakamani hapo.
0 Comments