Header Ads Widget

WAZIRI MASAUNI AMELIAGIZA JESHI LA POLISI KUFANYA KAZI KWA WELEDI

          Na Ashrack Miraji (Matukio  Daima   App)Lushoto

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni ameliagiza jeshi la polisi nchini kuendelea kulinda kiapo chake kwa kufanya kazi kwa weledi huku wakiishi  falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya  Maridhiano,Mabadiliko, Ustahimilivu na Kujenga Upya.


Waziri Masauni ametoa kauli hiyo wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakati akifungua kituo kipya cha polisi kilichojengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 400.


Amesema moja kati ya kazi kubwa za jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao,hivyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa karibu na wananchi kutaifanya jamii iendelea kuongeza ushirikiano.


Nao baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamesema wana imani kubwa na jeshi la polisi na wako tayari kuliunga mkono pindi watakapowahitaji kwa maslahi mapana ya Taifa.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI