Header Ads Widget

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA MFANYABIASHARA NDAMBO WAKAMATWA NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati Jeshi la Polisi mkoani Njombe likiwakamata watu 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kihalifu na mauaji katika kipindi cha mwezi Agosti mwaka huu watu wawili kati yao ni wanaohusika na mauaji ya aliyekuwa mfanyabiashara wa miamala ya fedha Godfrey Ndambo.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Ally Kitumbu amewataja wanaotuhumiwa kwa mauaji ya mfanyabiashara Ndambo kuwa ni Fanuel Seth Falo [24]  na Batista Filoteus Ngosso[30] Wote wakazi wa Makambako.


Aidha Kamanda Kitumbu amesema Jeshi la Polisi pia linawashikilia  Watu wawili Raia wa Kigeni Fikiri Omari Ken[40] na Humphery Nyairo[22]wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi wa kujitega kwenye taasisi za fedha na kufukuzia wateja kwa kutumia Gari wanaotoka na mabegi wakidhani ni fedha.


Amesema watuhumiwa hao wamekuwa na funguo za Bandia za magari ambazo wamekuwa wakizitumia kufungua magari ya watu na kuiba fedha na mali zinazokutwa kwenye magari hayo.


Hata hivyo Jeshi la Polisi linawataka wakazi wa Njombe kuacha tabia ya kukaa kimya pindi wanapokumbwa na majanga ya kuibiwa na kuporwa.


Kituo hiki kimezungumza na mmoja wa Waathirika wa kutapeliwa kupitia miamala ya simu ambaye anasema likatishwa tamaa na Jeshi la Polisi juu kufuatilia kesi yake jambo linalochagiza wengi kukaa kutoripoti matukio yanayowasibu.


Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Patrick Mhema na Elia Mguli wanasema licha ya Lawama nyingi kuelekezwa kwa Jeshi la Polisi lakini Jamii yenyewe inapaswa kukubali kuipokea elimu inayotolewa na Vyombo vya dola kwani bila hivyo Matukio yataendelea.


Matukio ya Barabarani pia yametajwa kusababisha Madereva  5928 Kukamatwa kwa makosa mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI