Header Ads Widget

MHASIBU, OFISA TEHAMA KANISA LA SDA WATUMIWA KUIBA SH. 717 MILION



Na matukio daima App,


Watu watatu wakiwemo Mhasibu na Ofisa Tehama wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (SDA), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka manane, likiwamo la kutakatisha fedha na wizi wa Sh717 milioni mali ya kanisa hilo.


Washitakiwa hao ni ofisa Tehema, Wilson Mapande (35) mhasibu, Winnie Owino (33) na mfanyabiashara, Nicolaus Owino (29).


Watatu hao wamefikishwa mahakamani hapo jana Septemba 25, 2024 na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga akishirikiana na Wakili wa Serikali, Aaron Titus.

Kabla ya kuwasomea mashitaka, hakimu Malewo alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Amesema mashitaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili washitakiwa hayana dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo wanatakiwa kusikiliza mashitaka na hawatatakiwa kujibu chochote.

Akiwasomea mashitaka, wakili Katuga amedai wanakabiliwa na mashitaka manane, la kwanza likiwa ni kuongoza genge la uhalifu, la pili wizi na la tatu hadi la nane ni utakatishaji fedha.

Katika shitaka la kwanza linalowakabili washitakiwa wote, amedai kati ya Mei 2021 na Januari 2023, waliongoza genge la uhalifu kisha kujipatia Sh717.126 milioni kutoka kwenye akaunti ya benki ya CRDB mali ya kanisa hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI