Header Ads Widget

WANANCHI NAMTUMBO WAIBUA NDEREMO NA VIFICHO, KWA RAIS SAMIA KUWAPELEKEA RUZUKU

 


Na Elizabeth Zaya

WAKULIMA wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, wamejikuta katika hali ya kupiga vifijo na nderemo, wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea ruzuku katika shughuli zao za kilimo

Walijikuta katika hali hiyo mbele ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aliyewatembelea akiwa katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Ruvuma katika eneo la Rwinga, Wilaya ya Namtumbo leo.

 Akizungumza baada ya kupokelewa na wananchi hao, Waziri huyo wa kilimo, Bashe alisema Rais Samia anastahili pongezi hiyo kwa kuwa amegusa maisha ya wannachi.

“Sisi wakulima tunapojiandaa kumpigia kura Rais Samia katika uchaguzi ujao, ni  kwa sababu amegusa maisha yetu. Huyu ndiye Rais ambaye amekuja madarakani na anampa ruzuku mkulima kuanzia shambani hadi sokoni, kwa maana mbegu, mbolea na hata zana za kilimo,” amesema Bashe.

Bashe amewataka wananchi hao kutumia vizuri ruzuku hiyo ili waendelee kunufaika na neema hiyo na kuleta tija katika shughuli zao hizo za kilimo.

Kadhalika, Bashe ametumia nafasi hiyo kutatua mgogoro wa ardhi inayomilikiwa na serikali chini ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) ambapo hapo nyuma alipatiwa mwekezaji kampuni ya NAFCO kuwekeza na baadae kuchukuliwa na serikali

“Niwashukuru wananchi kwa kuendeleza shamba hili na kupitia mhadhara huu “tuchimbe ngoko” kama wanavyosema wasukuma ili tuweke mambo sawa,” amesema Bashe.  

Pia, ameelekeza wakulima wagawiwe ekari 3000 na zilizobaki 3580 Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) atumie kulima mbegu bora, kuweka mashine ya kısasa ya kusafisha mbegu na ghala la kuhifadhia mbegu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI