WALIMU wa mchezo wa Judo nchini wametakiwa kuzingatia mafunzo ya mchezo huo ili kuandaa wachezaji wa timu ya Taifa.
Hayo yamesemwa na Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid wakati akifungua mafunzo ya siku 10 ya walimu wa mchezo huo nchini yanayoendeshwa na mkufunzi kutoka Uturuki Erdal Dogan, kwenye kituo cha Olympafrika Kibaha Mkoani Pwani.
Rashid amesema kuwa walimu hao wanapaswa kutumia mbinu watakazofundishwa kuibua vipaji vitakavyokuwa tegemeo kwa Taifa baadaye.
Kwa upande wake katibu wa TOC Filbert Bayi amesema kuwa kozi hiyo ni ya juu sana na muhimu hivyo walimu hao watasaidia kuzalisha wachezaji wengi na waipeleke mashuleni.
Naye Katibu wa Chama Cha Judo Innocent Mallya alisema kuwa mafunzo hayo ni ya siku 10 ambapo yanawashirikisha walimu 30 kutoka Bara na Visiwani ambapo mchezo huo unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vifaa.
0 Comments