Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
WANANCHI wa Mtaa wa Chidachi Kusini Dodoma wamemuomba Mbunge wa Jiji la Dodoma na Waziri wa Madini Anthony Mavunde kwa kushirikiana na ofisi ya jiji la Dodoma kuwapia maeneo yao ili kuendeleza ujenzi kwani limekuwa ni tatizo la muda mrefu.
Wakiongea na waandishi wa habari wananchi hao wamesema kuwa tangu mwaka 2018 waliahidiwa kuja kufanyiwa upimaji wa maeneo yao lakini kimekuwa kimya bila kuambiwa jambo lolote.
Magreth Dossa (66) Mkazi wa Chidachi Kusini amesema yeye ni Mkazi na mzaliwa wa eneo hilo tangu utoto wake wamekuwa wakizungushwa kwa muda wa miaka mingi lakini kupimiwa ni kama kitendawili kwao
" Mwaka 2018 walikuja kutuhakiki tukajua Mambo mazuri lakini hivi ninavyokwambia tangu miaka hiyo mpaka leo hatijapimi na hawasemi jambo lolote, "
Na kuongeza "Wenzetu wa Chidachi Senta wamepimiwa tunashangaa sisi kwanini hawajatufikia inamaana sio wa Tanzania, hatustahili kupimiwa timekuwa tukijiuliza maswali mengi majibu hakuna wakutujibu tuliambiwa tuandike barua lakini haikusaidia chochote, "
Naye Maria Mwanza amesema eneo hilo ni eneo la asili hivyo tunaiomba Serikali hasa mkurugenzi wa jiji la Dodoma
Frederick Sagamiko na team kuja Chidachi Kusini watupimie maeneo.
" Tunashindwa kuendeleza maeneo yetu hali inayotulazimu kulala na watoto wetu wakubwa katika chuma kimoja tunawafundisha nini hawa vijana wetu, " Amesema Mama huyu.
Issa Lazaro pia ni mkazi wa eneo hilo amesema shida ni kubwa katika Chidachi Kusini ni muda mrefu wamefuatilia kupimiwa lakini hakuna mafanikio maisha wanayoishi ni hatari kama familia kwani wanalazikika kulala na watoto wao.
"Tunamuomba Mama samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania ,Mkurugenzi wa jiji la Dodoma kutuona wananchi wa Chidachi tunahitaji upanuzi wa makazi tupimiwe tupate hati tuweze hata kukopesheka kwenye Taaasisi za kifedha, "Amesema
Naye Shabani Kayanda amesema tatizo hilo ni muda licha ya kuonesha jitihada zao lakiniafanikio hakuna na eneo linahuduma zote za kijamii ikiwemo Misikiti Makanisa bila kusahau umeme wa Rea sasa tunashangaa kwanini zoezi la upimaji linakuwa ni changamoto
" Eneo hili lilikuwa na Kaya zaidi ya 600 lakini limemegwa na kubakizwa eneo la Kaya 130 ambazo ndio tuliomo Sisi tunaoomba kupimiwa, "Amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Chidachi Kusini Mohamed Msanga alipofuatwa na kituo hiki amesema walichokisema wananchi ni yakweli kwani wameanza kuangaika nayo tangu mwaka 2014 kipindi cha CDA ambapo mwaka 2018 walikuja kupima kwa baadhi ya maeneo na kuacha Baadhi ya maeneo.
Amesema eneo linawatu wengi na wamejenga nyumba za maana kabisa lakini hawana hati kila siku tumekuwa tukitembea na bahasha kwenda jiji majibu yao ni wametenga maeneo hayo kwa shughuli za Serikali
" Eneo linawazi 130 wamejenga nyumba nzuri hawana hati hali inayoikosesha Serikali mapato tangu mwaka 2018 kwa kuzembea kufanya upimaji, "Amesema Mwenyekiti huyo
Amesema Tatizo hilo liliachwa na Mamlaka ya Ustawishaji na Mipango Miji CDA ambapo wametuachia mgogoro na ukieenda jiji ukisema umepimiwa na CDA haupatiwi
Hata hivyo kufutia sakata hilo alitafutwa
Maduhu Ilanga Mkuu wa Divisheni wa uendelezaji wa makao makuu lakini hakupatikana simu yake iliita bila kupokelewa.
0 Comments