Header Ads Widget

WAKUU WA SHULE JIMBO LA SAME MASHARIKI WAMUAHIDI MBUNGE UFAULU MKUBWA



NA WILLIUM PAUL, DODOMA. 



WAKUU wa shule za Sekondari na Makamu wao kutoka katika Jimbo la Same mashariki wamemuhakikishia Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango Malecela shule za Sekondari kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.



Walimu hao wametoa ahadi hiyo walipofanya kikao na Mbunge huyo walipowasili jijini Dodoma kwa mwaliko kutoka kwa Mbunge huyo kushiriki Bungeni kujionea na kujifunza shughuli za Bunge zinavyoendeshwa. 



Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Taaluma wilaya ya Same ambaye pia ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kwa mbegu, Godwine Kitale alisema kuwa, mwaliko huo wa kushiriki Bungeni wao kama walimu watautumia kama chachu ya kusukuma ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa. 



"Shule yoyote inayofanya vizuri tunapaswa kutambua mtu pekee aliyesababisha hilo ni Makamu Mkuu wa shule hawa ni watu muhimu sana katika kuinua ufaulu na nikupongeze sana Mbunge kwa kuitambua dhamani yao na kupitia hili tunategemea kuona ufaulu ukiongezeka katika Jimbo letu" Alisema Kitale. 



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI