Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI NA MACHIFU TUMIENI MIKUSANYIKO KUKUMBUSHA WAZAZI WAJIBU WA MALEZI KWA WATOTO

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga


Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Beno Malisa

Na  Matukio Daima App,Mbeya

SERIKALI mkoani Mbeya imewaomba viongozi wa dini na machifu kutumia mikusanyiko ya  watu kuwakumbusha wajibu wao hususan  wazazi na walezi kuzungumza na watoto  na kuwakagua   ili waweze kubaini  kama wamefanyiwa vitendo vya ukatili.

Kauli hiyo imetolewa  leo  Jumatano Septemba 25,2024 na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya , Beno Malisa kwa niaba ya  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya “Tuwaambie kabla hawajaharibiwa “iliyowalenga wanafunzi wa shule za msingi ,sekondari pamoja na wanafunzi wa vyuo.

“Niwaombe watoto tukatoe ushirikiano mzuri kwa wazazi lakini na wazazi mkatimize wajibu wenu wa msingi tunadaiwa kwenye taratibu zetu kwenye malezi na malezi yetu hivyo tufuate misingi  na taratibu zetu kwa watoto tunaowaleta duniani “amesema Mkuu huyo wa Wilaya .

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwatahadharisha vijana na watoto wa umri rika  changamoto ambazo zinawakabiri  pamoja na mazingira wanayokulia na kuitaka jamii kuitumia kampeni hiyo kupeleka elimu kila kona na kuhakikisha wanaondoa mmonyoko wa maadili unaoinyemelea jamii .

“Mmonyoko huo upo kundi la watoto ambalo halijaweza kujitambua kwa asimilia 100, na kuhitaji usaidizi wa walezi ,walimu na jamii kwa ujumla ili wawe watoto salama na Taifa la leo pamoja na  kesho.

Amesema  Mkoa wa Mbeya wamejizatiti kuhakikisha elimu ya ukatili wa kijinsia inafika kila mahali na kuwa hawatasita kwa mtu yeyoye ambaye atakuwa kinyume na kampeni hiyo na wale ambao wataendeleza tamaduni zisizo sawa kwa watoto na kuonyesha nia ya kutekeleza lengo la unyanyasi wowote au kutimiza azima inayopelekea ukatili wa kijinsia kwa watoto na kwamba sheria na taratibu zipo wazi.

Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya ,Benjamin Kuzaga amesema kuwa Kampeni hiyo ya Tuwaambie kabla hawajaharibiwa kitaifa ilizinduliwa mkoa wa  Njombe Agosti 29,2024 na kuwa mkoa wa Mbeya imezinduliwa leo ambapo kwa wilaya zote walishazindua kampeni hiyo.


Kamanda Kuzaga amesema lengo la kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuwalinda wanafunzi na watoto wadogo na kwamba  imeanzishwa kwa ajili ya kusaidiana na wazazi ,walimu na walezi ili kuweza kuwalinda watoto na kupata taarifa za watu ambao wanahusika na vitendo vya kubaka ,vipigo ambavyo vinawaathiri watoto .

Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoa Mbeya ASP, Veroca Ponela amesema kampeni hiyo itaendelea kutolewa katika shule za msingi , Sekondari , vyuo vya kati na vyuo vya elimu ya juu lengo likiwa ni kupinga ukatili unaoendelea katika jamii watoto wengi hawajitambui na baada ya kutoa elimu watajitambua na wakifanyiwa watatoa taarifa.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI