Header Ads Widget

SIKU HIZI MJOMBA SIO MAMA USIKUBALI ALALE NA MTOTO NDANI"MWACHUĹA"

Na Shomari Binda-Musoma 

KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara Baraka Mwachura amesema wazazi wasikubali wajomba wa watoto wao kulala nao chumbani.

Licha ya wajomba wageni wanaowatembelea sio vyema kukubali kuwalaza chumba kimoja na jinsi tofauti bali watoto walale peke yao.

Hayo ameyasema leo mei 20,2025 ofisini kwake alipokuŵa akizumzia kukamilika kwa ziara ya kuangalia uhai wa jumuiya hiyo na chama kwenye Wilaya za Rorya,Bunda,Butiama,Musoma mjini na Wilaya ya kichama ya Musoma vijijini.

Amesema matukio ya ulawiti na ubakaji yamekuwa yakiripotiwa na kutokea kwenye familia hivyo tahadhari zinapaswa kuchukuliwa na wazazi majumbani.

Mwachula amesema sio wajomba au ndugu wote wanaoaminika na kuwapa nafasi ya kulala na watoto ndani wengine wamekuwa wakiwafanyia vitendo vibaya.

Amesema watoto wamekuwa wakiingiliwa na wengine hawasemi matokeo yake wanaharibikiwa na kuwa na kizazi kisichofaa.

Katibu huyo amesema katika ziara yaķe aliyofanya  kwenye ziara kwenye Wilaya hizo licha ya mambo mengine ya kuhimiza uhai wa jumuiya na chama amesisitiza suala la mmomonyoko wa maadili.

" Kwenye ziara nimewaambia kwa sasa mjomba sio mama hiyo ilikuwa zamani wazazi wasikubali wallet na watoto chumba kimoja.

" Na hii sio kwa wajomba peke yao bali kwa wageni wote wanaokuwa wanawatembelea majumbani wawatafutie sehemu nyingine ya kulala sio na watoto",amesema.

Amesema katika ziara aliyoifan̈ya licha ya kusisitiza jambo hilo yapo maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wa jumuiya aliokutana nao ikiwa ni pamoja na ya kuzingatia kuelekea uchaguzi mkuu.

Moja ya mambo ni kujiepusha na wagombea watakaokuja kuomba nafasi kwa kutoa Rushwa kwa kuwa Rushwa inadhalilisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI