Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga
Mkuu wa wilaya ya Mbeya,Beno Malisa
Na Matukio Daima App,Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imewaomba viongozi wa dini na machifu kutumia mikusanyiko ya watu kuwakumbusha wajibu wao hususan wazazi na walezi kuzungumza na watoto na kuwakagua ili waweze kubaini kama wamefanyiwa vitendo vya ukatili.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Septemba 25,2024 na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya , Beno Malisa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya “Tuwaambie kabla hawajaharibiwa “iliyowalenga wanafunzi wa shule za msingi ,sekondari pamoja na wanafunzi wa vyuo.
“Niwaombe watoto tukatoe ushirikiano mzuri kwa wazazi lakini na wazazi mkatimize wajibu wenu wa msingi tunadaiwa kwenye taratibu zetu kwenye malezi na malezi yetu hivyo tufuate misingi na taratibu zetu kwa watoto tunaowaleta duniani “amesema Mkuu huyo wa Wilaya .
Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwatahadharisha vijana na watoto wa umri rika changamoto ambazo zinawakabiri pamoja na mazingira wanayokulia na kuitaka jamii kuitumia kampeni hiyo kupeleka elimu kila kona na kuhakikisha wanaondoa mmonyoko wa maadili unaoinyemelea jamii .
“Mmonyoko huo upo kundi la watoto ambalo halijaweza kujitambua kwa asimilia 100, na kuhitaji usaidizi wa walezi ,walimu na jamii kwa ujumla ili wawe watoto salama na Taifa la leo pamoja na kesho.
Amesema Mkoa wa Mbeya wamejizatiti kuhakikisha elimu ya ukatili wa kijinsia inafika kila mahali na kuwa hawatasita kwa mtu yeyoye ambaye atakuwa kinyume na kampeni hiyo na wale ambao wataendeleza tamaduni zisizo sawa kwa watoto na kuonyesha nia ya kutekeleza lengo la unyanyasi wowote au kutimiza azima inayopelekea ukatili wa kijinsia kwa watoto na kwamba sheria na taratibu zipo wazi.
Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya ,Benjamin Kuzaga amesema kuwa Kampeni hiyo ya Tuwaambie kabla hawajaharibiwa kitaifa ilizinduliwa mkoa wa Njombe Agosti 29,2024 na kuwa mkoa wa Mbeya imezinduliwa leo ambapo kwa wilaya zote walishazindua kampeni hiyo.
Kamanda Kuzaga amesema lengo la kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuwalinda wanafunzi na watoto wadogo na kwamba imeanzishwa kwa ajili ya kusaidiana na wazazi ,walimu na walezi ili kuweza kuwalinda watoto na kupata taarifa za watu ambao wanahusika na vitendo vya kubaka ,vipigo ambavyo vinawaathiri watoto .
Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoa Mbeya ASP, Veroca Ponela amesema kampeni hiyo itaendelea kutolewa katika shule za msingi , Sekondari , vyuo vya kati na vyuo vya elimu ya juu lengo likiwa ni kupinga ukatili unaoendelea katika jamii watoto wengi hawajitambui na baada ya kutoa elimu watajitambua na wakifanyiwa watatoa taarifa.
Mwisho
0 Comments