Header Ads Widget

TANZANIA NA COMORO WASAINI HATI YA MASHIRIKIANO USIMAMIZI WA BAHARI

 







Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) leo kimetiliana saini hati ya mashirikiano na shirika la kitaifa la masuala ya Bahari la Muungano wa Comoro (ANAM) kwa lengo la kujenga rasilimali watu na kupata mafanikio makubwa kwenye sekta ya bahari.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkuu wa DMI, Dkt Tumaini  Gurumo amesema kuwa wapo tayari kufanya kazi na Comoro ikiwa ni kuwapatia mafunzo namna ya usimamizi wa meli ili kuhakikisha sekta ya maji wanakwenda nayo pamoja.


Amesema kuwa, Comoro ni kisiwa kilichozungukwa na maji, matumizi ya maji kwao ni makubwa na maji yanahitaji usimamizi, pia wana meli nyingi wamesajili meli 300 lakini hawana ujuzi mzuri wa kuzisimamia hivyo wakiweza kupatiwa mafunzo na DMI yataweza kuwasaidia katika kuziendesha meli hizo.


"Ni wakati wa vijana wetu na Comoro kuiona hii fursa ya uwekezaji katika sekta ya bahari, chuo cha DMI ni chuo bora ambacho kinatoa mafunzo na miongozo inayohitajika kimataifa, tumekidhi vigezo njooni mupate mafunzo na ujuzi katika usimamizi wa bahari "amesema Dkt Tumaini.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kitaifa la masuala ya Bahari la Muungano wa Comoro ANAM, Mohamed Said Salim Dahalani amesema kumekua na Ushirikiano makubwa kati Tanzania na Comoro ambapo zaidi ya asilimia 80 ya Biashara zao huchukuliwa Tanzania kwa kutumia meli.


Amesema kuwa, Tanzania wana uwezo mzuri wa usimamizi wa bahari kuliko Comoro hivyo makubaliano hayo yataleta tija sana kwa pande zote mbili kwani wanafunzi wanaotoka Comoro wanaosoma DMI wamekuwa wakifanya vizuri katika masuala ya usimamizi wa bahari ikiwemo meli, nchini kwao.


"Sisi tumezungukwa na barahari nchi yetu ni kisiwa lakini wa Comoro hawaoni umuhimu wa bahari, tutawaambia waje huku wasome wapate ujuzi ili washiriki vizuri kwenye mambo ya bahari ikiwemo kuendesha meli, tuna meli nyingi lakini hatuna ma engineer wala captain"amesema Dahalani.


Ameongeza kuwa, kutokana na ukosefu wa ujuzi wa usimamizi wa bahari na meli wamekuwa wakipoteza biashara nyingi, hivyo kupitia Ushirikiano huo utasababisha kupata miongozo ya namna ya kuendesha biashara zao vizuri bila kupotea wala kuharibika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI