Header Ads Widget

SHULE YA MSINGI INAKABILIWA NA TATIZO LA VYOO, WALIMU WANAJISAIDIA SHULE JIRANI


Wanafunzi wa darasa la saba waliohitimu shule ya msingi Kigoma Mwaka huu wakiwa kwenye mahafali ya kumaliza darasa la saba
Afisa Tawala wa wilaya Kigoma Dolla Buzaire (wa pili kulia) akikabidhi cheti cha kuhitimu darasa kwa mwanafunzi Luqman Fadhili  (kushoto) katika mahafali ya shule hiyo (kulia) Mwalim Mkuu wa shule ya msingi Kigoma Bujaga Simon

Bujaga Saimon Mwalim Mkuu shule ya Msingi Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Shule ya Msingi Kigoma iliyopo katika manispaa ya Kigoma Ujiji katikati ya Mji wa  Kigoma  inakabiliwa na changamoto kubwa ya vyoo hali inayowalazimu walimu wa shule hiyo kujisaidia katika shule Jirani.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Bujaga  Simon alisema hayo mbele ya Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji,Mgeni Kakolwa na Afisa Tawala wa wilaya Kigoma,Dola Buzaire aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya Kigoma katika mahafali ya darasa ya saba ya shule ya Msingi Kigoma.

Mwalim Simon alisema kuwa mwezi Februari mwaka huu vyoo vya wasichana katika shule hiyo vilibomka kutokana na mvua kubwa hivyo ikalazimu walimu kutoa vyoo walivyokuwa wanatumia ili vitumiwe na wanafunzi wasichana Zaidi ya 400 na walimu kuomba na kuanza kujisaidia katika shule Jirani.

Pamoja na hilo Mwalim Simon alisema kuwa pia shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa uzio na hasa kwa sababu iko katikati ya mji kwenye shughuli nyingi hivyo shule hiyo imekuwa mapito ya watu na kuhatarisha mali za shule hiyo usalama wa wanafunzi.

Akijiibu maneno hayo ya Mkuu wa shule kuhusiana na changamoto ya vyoo na uzio Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mgeni Kakolwa alisema kuwa atafikisha ujumbe huo kwa Meya wa mansipaa ya Kigoma Ujiji, Baraka Lupoli ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi akiwa pia ndiyo diwani wa kata hiyo ya Kigoma.

Pamoa na hilo Kakolwa alisema kuwa ni wazi changamoto hiyo inahitaji utatuzi wa haraka hivyo yeye kama Naibu Meya atashauriana na Meya na uongozi wa manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia kwa Mkurugenzi kuona changamoto hiyo inamalizwa haraka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI