Header Ads Widget

DPP ASHINDA KESI LA GARI V8 LILILOBEBA WAHAMIAJI HARAMU


SAKATA la Raia wa Tanzania anayeishi Afrika Kusini, Jackson Ngalya anayedai gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 namba T888 BTY lililokamatwa na wahamiaji haramu mjini Moshi ni mali yake limekwama baada ya Mahakama kutupa maombi yake.

Mahakama imekubali hoja mbili kati ya tatu za pingamizi lililowekwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kutokana na dosari za kisheria alizobaini katika maombi hayo namba 21838 ya mwaka 2024.

Gari hilo lilikamatwa Juni 4, 2024  Njipanda ya Himo, likiwa na wahamiaji haramu saba, raia wa Ethiopia waliokuwa wakisafiri kuelekea Afrika Kusini, ambao baadaye walitiwa hatiani na kuhukumiwa kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja au kifungo cha mwaka mmoja jela.


Tangu kukamatwa kwa gari hilo na baadaye Mahakama kukubali litaifishwe kuwa mali ya Serikali baada ya kukubali ombi la DPP, hakuna mtu aliyejitokeza kudai ni mmiliki hadi Julai 31, 2024 alipojitokeza Ngalya.

Gari hilo liliingizwa na kusajiliwa mwaka 2011 kwa jina la mbunge mmoja wa CCM lakini umiliki ukahama Juni 24, 2024 kwenda kwa Ngalya ikiwa ni baada ya kupita siku 20 tangu likamatwe na umefanyika likiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

Hili liliibua maswali mengi yasiyo na majibu ya namna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilivyoruhusu uhamisho wa gari ambalo ni kielelezo cha kesi.

Katika kiapo cha maombi dhidi ya DPP na raia hao saba wa Ethiopia, Ngalya alidai kuanzia mwaka 2016 hadi sasa, amekuwa akiishi Afrika Kusini na kwamba gari hilo aliliacha nyumbani kwake nchini Tanzania, chini ya uangalizi wa mlinzi.

Kwa mujibu wa kiapo hicho, Juni 2024 alijulishwa kuwa gari lake halijulikani lilipo, hivyo Juni 3, 2024 alikwenda Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kutoa taarifa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI