Na Matukio Daima App,Mwanza
Mkurugenzi wa Shule ya Santa Edwin English Medium Bwana Edwin Soko iliyopo Majengo Mapya - Nyegezi Kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza amesema shule hiyo itaendelea kutenga nafasi nyingi zaidi za kusaidia watoto wanaotoka kwenye familia zenye changamoto za kipato kuendelea kusoma chini ya ufadhili wa Shule.
" Ndugu Mgeni rasmi Kwa sasa shule inafadhili watoto ishirini na itaendelea kuongeza idadi ya wanafunzi hao" alisema Mkurugenzi Edwin Soko.
Soko aliongeza kuwa, ndoto yake ya kuisaidia jamii imetimia Kwa kuwa sasa Santa Edwin English Medium ipo na inaendelea kuhudumia jamii Kwa kutoa elimu bora.
" Santa Edwin English Medium tunaendeleza maono ya Rais wetu Mama Samia Kwa kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora pamoja na kulinda utu wake" alisema Edwin Soko, Mkurugenzi wa Santa Edwin English Medium School.
Soko alisema kuwa Santa Edwin inaendelea kufanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali kwani Kwa Mwaka huu mtihani wa utimamu wa darasa la nne (Mock) Mkoa shule ilishika nafasi ya 15 Kati ya shule 151 na mtihani wa kata imeshika nafasi ya kwanza.
Naye Mkuu wa Shule Bwana Hassan Mussa amesema.kuwa anawashukuru wazazi Kwa wote Kwa kuwaleta watoto kusoma hapo na amewaomba waendelee kuiamini shule hiyo.
0 Comments