Header Ads Widget

JESHI LA POLISI LAWEKA MKAZO "MARUFUKU MAANDAMANO YA CHADEMA"

 

WAKATI mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akitangaza uwepo wa Maandamano ya Chama hicho Siku ya jumatatu September 23 ,Jeshi la Polisi Nchini limeweka mkazo wake kuwa piga marufuku   maandamano hayo .

Kuwa maandamano hayo yana viashiria vyote vya uvunjifu wa amani Nchini.K

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro  ametoa Kauli hiyo leo Jumapili Septemba 22.2024) kuwa  Jeshi hilo lilipokea taarifa ya chama hicho kuhusu dhamira ya kufanya maandamano hayo, taarifa ambayo ilijibiwa kwa kuelezwa kuwa maandamano husika yamepigwa marufuku hivyo yeyote atakayefanya kinyume na hapo atashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria

Hata hivyo alisema  kumekuwa na kauli zinazoashiria wazi kuwa maandamano hayo yana lengo la kuvuruga amani nchini kutokana na kauli tofauti zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA na kwamba Jeshi la Polisi kama wasimamizi wa sheria na wenye jukumu la kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao (amani) hawako tayari kuruhusu kufanyika kwa matukio ya namna hiyo


Maandamano yale yamepigwa marufuku, wao wametoa taarifa na sisi tumewapa taarifa, kwa hiyo wakifanya kinyume sasa tutachukua hatua kali za kisheria za kuyazuia na kushughulika na watu watakaojihusisha na maandamano hayo vikali na kwa mujibu wa sheria" -SACP Muliro

Hata hivyo  Muliro aliwataka wananchi kutohudhuria maandamano hayo kwa kuwa yamepigwa marufuku, na kwamba marufuku hiyo imetokana na kauli na matamko ynayotolewa na viongozi wa chama hicho hivyo kudai kuwa maandamano hayo hayatakuwa ya amani kama inavyoelezwa badala yake dhamira ya maandamano hayo ni kuvuruga amani

"Jeshi la Polisi kama taasisi tumeshatoa tamko kwamba watu wasishuriki, wasijitokeze kwenye maandamano hayo, lakini watu wema waendelee na shughuli zao za kawaida mbalimbali za ujenzi wa Taifa, ujenzi wa kiuchumi na masuala mengine ambayo yanasaidia watu kujenga ustawi wa maeneo yao" -SACP Muliro


Mapema leo Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)Taifa Freeman Mbowe kupitia mitandao ya kijamii akisisitiza uwepo wa maandamano kesho jumatatu  .

Mbowe ametoa Msimamo huo wakati akizungumzia Msimamo wa CHADEMA  kupitia 'X space' leo, Jumapili Septemba 22.2024 Mbowe amesema kuwa maandamano hayo yatahusisha njia mbili ambazo ni Magomeni kupitia Barabara ya Morogoro mpaka viwanja vya Mnazi mmoja na njia ya pili ni ile inayotoka Ilala Boma Sokoni kupitia Barabara ya Uhuru mpaka viwanja vya Mnazi mmoja, ambapo kwa lugha rahisi viwanja vya Mnazi mmoja ndipo sehemu ya makutano ya maandamano hayo

Mbowe amesema maandamano hayo yanatarajiwa kuanza majira ya saa 03 asubuhi, hivyo kutoka wito kwa wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla wake kujitokeza kwa wingi kushiriki bila woga wowote kwa kuwa maandamano hayo ni ya amani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI