Header Ads Widget

MWANARIADHA WA KIMATAIFA ATOA SOMO KWA WANAFUNZI ZANZIBAR

 





NA  MATUKIO DAIMA APP ZANZIBAR

WANAFUNZI wameshuriwa kujiwekea malengo ya kitaaluma mara baada ya kumaliza elimu sambamba na kuwa ushirikiano ili kujenga jamii iliyo bora.

Ushauri huo umetolewa na mwanariadha wa kimataifa wa Grenad, Lindon Victor, alipokuwa akizungumza na wanamichezo wa Sekondari ya Ben Bella na Haile Salassie jana.

Alisema, ni muhimu kwa wanafunzi hao kujipangia mustakbali wa maisha yao ya mbeleni na kuzingatia ushauri wa watu wenye malengo ya maendeleo na kuacha kushirikiana na watu wenye mitazamo iliyokosa malengo.

Alisema, wanafunzi wanapokuwa wameweka malengo iwe ya kimasomo au kimichezo wanakuwa wametengeneza hatma bora kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

"Kwa dunia ya sasa elimu ndiyo kila kitu, lakini, msisahau michezo nayo ina fursa nyingi ya kufanikiwa kimaisha.

"Kati yetu wapo wanafunzi ambao hawatobahatika kuendelea na elimu ya juu zaidi, lakini, michezo pia ina sehemu kubwa ya maisha bora", alisema, mshindi huyo wa medali ya dhahabu ya michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Mwanaridha huyo aliwatolea mfano wa yeye mwenye ambapo alisema, alikulia katika familia masikini, lakini, michezo ndiyo iliyomuondoa kwenye umasikini huo na sasa akiwa na jina kubwa duniani.

"Wazee wangu walikuwa masikini na mimi niliishia nikiwa nachunga mifugo, lakini, niliweka malengo ambayo yameniwesha kufika hapa nilipo sasa".

Kwa Rais Waziri wa Michezo wa Sekondari ya Haile Salassie, Ally Abdul Ally, aliwashauri wanafunzi wenzake kuendeleza mashirikiano baina yao na walimu ili kufikia malengo yao waliyojiwekea iwe ya kielimu au kimichezo.

Lakini pia aliwashauri kutokubali kupokea ushauri ambao utawaweka nje ya matarajio yao ya baadae.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI