NA NAMNYAK KIVUYO, LONGIDO
Warizi wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Mohamed Mchengerwa amesikitishwa na kutokakamika kwa mradi wa ujenzi wa ujenzi wa Bwalo na Madarasa katika shule mpya maalum ya sekondari ya wasichana ya Samia iliyopo wilayani Longido ambapo amemuonya mkurugenzi wa Wilaya ya Longido Nassoro Shemzigwa kutokana na kumdanganya pamoja na kuagiza ujenzi huo kukamilika ifikapo Novemba 1,2024.
Mchengerwa ametoa agizo na onyo hilo katika ziara yake shuleni hapo kutokana na kuchelewa kukamilika kwa mradi huo ambapo alisema kuwa amesikitishwa na kutokamilika kwa mradi huo ulioanza kutekelezwa Septemba 30,2023 na ulitakiwa kukamilika Septemba 30, 2024 jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani.
Alieleza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anataka kunyanyua maisha ya watoto wa kike na kutengeneza wanasayansi wapya katika nchi ambapo ametoa fedha kwa asilimia 100 ambazo ni Bilioni 108 kwa nchi nzima huku kila mkoa ukipokea Bilioni 4.6 kwaajili mradi huo.
"Fanyeni kazi usiku na mchana Bwalo likamilike na wanafunzi waanze kulitumia, Mkurugenzi umenidanganya, nakupa muda wa kujirekebisha,usirudie tena lakini hii haihusiani na taarifa ya TAKUKURU nikishaipata hatua stahiki zitachukuliwa ila kwasasa ninachoagiza ni mradi uwe umekamilika ifikapo November 1,2024, kwani inaonekana mradi huo haujakamilika kwasababu kuna watu wanachomoa chomoa fedha," Alisisitiza Mchengerwa.
" Mradi huu utatengeneza fursa kwa watoto wa kike kupitia sayansi ,nimesikitishwa sana kuona haujakamilika, huu ni uzembe na ujumbe uende kwa mikoa yote nikipita nataka kuona mradi umekamika na wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri,Alisema.
Aidha alimtaka mkuu wa wilaya hiyo Salum Kali kutokaa ofisini badala yake aige utendaji wa mkuu wa mkoa Paul Makonda wa kutembea na kusikiliza changamoto za wananchi ikiwa ni pamoja na kumpa taarifa za utekelezaji wa umaliziaji wa mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda alisema kuwa aliagiza TAKUKURU wafanye uchunguzi latika mradi huo ambapo wamemtumia akiwa njiani kuelekea katika shule hiyo leo ambapo kwa haraka haraka ameona kuna fedha zilizotumika nje ya utaratibu.
"Katika Taarifa ya TAKUKURU Mh Waziri nimeona kuna bilioni 1 imelipwa kwa wazabuni bila risiti za EFD lakini pia milioni 300 zimelipwa bila kuwepo kwa nyaraka zozote na asilimia 71 ya wazabuni iliongezwa kinyume cha utaratibu,ninaomba niipitie taarifa hii vizuri alafu niilete kwako,"Alieleza Makonda.
Naye mkuu wa shule wa shule hiyo Esther Kobelo awali mradi huo ulikuwa na gharama ya shilingi Bilioni 3 ambazo Zilipokelewa na zote zimetumika kwa awamu ya kwanzwa na baadae kuongezewa Bilioni 1.4 kwaajili ya ukamishaji wa Bwalo na miundombinu ambapo utekelezaji utaanza baada ya utaratibu wa manunuzi kukamilika na hadi sasa mradi umefikia utekelezaji wa asilimia 90.5.
0 Comments