MWENYEKITI WA IRINGA MOTOR SPORT CLUB, HOODY MASASI
Na matukio daima App,
Mwenyekiti wa Iringa Motor Sport Club, Hoody Masasi amewakaribisha wananchi mkoani Iringa kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya magari yaliyopewa jina la Euro Cables Liqui Moly yatakoyafanyika kuanzia tarehe 14 hadi 15 mwezi huu.
Mwenyekiti huyo amesema hayo, wakati akimkaribisha, msimamizi wa mchezo huo ili aelezee hatua walizofikia katika maandalizi ya mchezo huo.
HIDAYA KAMANGA MSIMAMIZI WA MCHEZOKwa upande wake, msimamizi wa Mashindano hayo Hidaya Kamanga, amesema mashindano hayo ya kilomita 126 ambayo yatafanyika katika shamba la MT Katika kijiji cha Mangalali wilaya ya Iringa, kwa sasa maandalizi yake yamefikia asilimia 90.
Aidha, Kamanga, amewatoa hofu mashabiki watako jitokeza katika upande wa usalama kwa vyombo vyote vya usalama vitakuwepo pamoja na taasisi zote zinazohusika na mchezo huo.
MBUNGE WA IRINGA MJINI JESCA MSAMBATAVANGU
Kwa upande wake Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msambatavangu, amewapongeza waandaji wa mashindano hayo kwa kuendelea kuutangaza mkoa huo pamoja na kuukuza kiuchumi, ikiwemo utalii wa kusini.
Amesema kuwa mchezo wa mashindano ya magari, umekuwa ni nembo ya mkoa wa Iringa jambo ambalo linatangaza vyema mkoa pamoja na nchi kwa ujumla, hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi hizo ambazo zinatumia gharama kubwa katika maandalizi yake
"Ni waombe wananchi wa mkoa wa Iringa mjitokeze kwa wingi ili kuwaunga mkono wawekezaji hawa, maana wanatumia gharama kubwa lakini kila siku hawakati tamaa"alisema Msambatavangu.
0 Comments