Header Ads Widget

MADIWANI KASULU KUENDESHA VIKAO KIDIJITALI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imegawa vishikwambi  (tablets) kwa madiwani wa halmashauri hiyo ikiwa ni kutekeleza mpango wa serikali wa kuchochea matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika utekelezaji wa majukumu ya umma na vikao.


Jumla ya vishikwambi 70 vimenunuliwa na kugawiwa kwa  madiwani wa halmashauri hiyo  sambamba na Kamati ya Uinzi na Usalama ya Wilaya ya Kasulu, wakuu wa divisheni na vitengo pamoja na baadhi ya viongozi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yaWilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus Mashimba akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza hilo la madiwani amesema kuwa ugawaji wa vishikwambi unaenda kuifanya halmashauri  kuendesha vikao  vya mabaraza yamadiwani badala ya kutumia makabrasha.


Akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Kasulu,  Eliya Kagoma amesema kuwa vifaa hivyo vitaleta matokeo chanya kwa kurahisisha upatikanaji wa taarifa pamoja na kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika kwenye uandaaji wa makabrasha.


Naye Mwenyekiti wa Chama Cha MapinduziWilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe  amesema kuwa  jiografia ya halmshauri hiyo ina eneo kubwa la kiutawala hivyo ununuzi wa vishikwambi hivyo  utapunguza gharama za uendeshaji na fedhazilizokuwa zinatumika kuandaa makabrasha zitakwenda kusaidia utekelezaji miradi mingine ya maendeleo.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI