Header Ads Widget

DCPC WALAANI POLISI KUWAPIGA NA KUKAMATA WAANDISHI WA HABARI KWENYE MAANDAMANO YA CHADEMA,DAR ES SALAAM,DCP MISIME AFAFANUA.....



KUFUATIA kitendo Cha jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kuwakamata waandishi wa habari waliokuwa wakitimiza wajibu Wao kuripoti habari za maandamano ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Jana mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) Samson Kamalamo ametoa tamko kali kupinga unyanyasaji huo dhidi ya waa dishi wa habari .

 Kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo September 24/2024 Kamalamo amesema DCPC  imepokea kwa masikitiko makubwa vitendo vya kushambuliwa na kunyanyaswa kwa waandishi wa habari vilivyotekelezwa na askari wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum Dar es Salaam, tarehe 23 Septemba, 2024, jijini Dar es Salaam. 

Kuwa waandishi hao walikuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi wakati wa maandamano yaliyoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Aliwataka waandishi walioshambuliwa ni pamoja na Peter Filipo Mhogo na Marium Mbegu wa East Africa TV, Baraka Loshilaa, Lawrence Mnubi, na Michael Matemanga wa Mwananchi Communications, pamoja na Agustina, Ofisa Habari Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

"Waandishi hawa walikamatwa katika eneo la Ilala Boma wakiwa wanasubiri usafiri baada ya kufukuzwa kutoka eneo hilo. Licha ya kujitambulisha kuwa ni waandishi wa habari na wengine wao wakiwa wamevaa mavazi rasmi ya utambulisho (Press Jacket), walishambuliwa na kukamatwa"

 Mmoja wa waandishi hao alipigwa na kukanyagwa mgongoni akiwa ndani ya gari la polisi maarufu kama "Defender," hali iliyomsababishia maumivu makali ya mgongo.

Alisema kuwa waandishi hao walipofikishwa katika vituo vya Polisi vya Msimbazi na Buguruni, walinyang'anywa vitendea kazi, vitambulisho vya kazi vya ofisi walizotoka, na kadi za utambulisho wa waandishi wa habari (Press Cards). Hata hivyo, baada ya muda waandishi hao waliachiwa baada ya kupigwa picha wakiwa wameshika vitambulisho vyao.

"DCPC inalaani kwa nguvu zote vitendo hivi na inalitaka Jeshi la Polisi kurejea katika makubaliano ya pamoja ya ushirikiano katika utendaji kazi, ambayo yalifikiwa kati ya Jeshi la Polisi na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC) Makubaliano haya yanakusudia kuhakikisha mazingira salama ya utendaji kazi kwa waandishi wa habari"

Kamalamo alisema kuwa vitendo vya aina hii havipaswi kurudiwa, hasa tunapoelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. DCPC inatoa wito kwa uchunguzi wa kina kufanyika, na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya askari polisi waliohusika na vitendo hivi vya kinyama.

Akijibu swali la Frank Leonard mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Jana wakati wa  mkutano wa kujadili usalama wa waandishi wa habari Nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa kuandaliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kuhusu sababu ya kukamatwa kwa waandishi wakiwa kwenye Majukumu yao kufuatilia maandamano ya CHADEMA kama ni kosa ama lah.

Msemaji wa polisi Nchini DCP David Misime alisema kuwa Bado Kuna haja ya polisi kutoa majibu sahihi ya waandishi hao kukamatwa .

Akijibu hoja hizo DCP Misime alisema kuwa polisi hawakamati bila sababu lazima kamatakamata yoyote Ina sababu yake.

Kuhusu Suala la waandishi wawili waliodaiwa kukamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA leo alisema hata weza kutolea majibu Kwa sasa pasipo kujua sababu ya kukamatwa kwao .

Japo alisema si kosa kwa waandishi wa habari kuripoti habari za maandamano na ndio maana hakuna sehemu yoyote ambayo jeshi la polisi limetoa Kauli ya Kuzuia waandishi kuripoti maandamano nchini .

DCP Misime alisema kuwa jeshi la polisi linafanya kazi kwa weledi na kuwa hawafanyi kazi kwa mihemuko wala kutekeleza maelekezo ya Chama chochote Cha siasa .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI