NA WILLIUM PAUL, DODOMA.
MABINGWA wa michuano ya Mkenda cup klabu ya Rongai FC imepokea kipigo cha magoli mawili kwa moja kutoka kwa wenyeji wao timu ya Fountain gate high school katika uwanja wa Fountain gate arena jijini Dodoma.
Mtanange huo ulioanza majira ya jioni ulikuwa na ushindani mkubwa huku kukishuhudiwa kila mmoja akitafuta goli hadi kipindi cha kwanza kinakamilika Fountain gate walikuwa wakiongoza kwa magoli mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa na kupelekea Rongai FC kupata goli la kufutia machozo na hadi dakika tisini zinakamilika matokeo yalikuwa magoli mawili kwa moja.
Mchezo huo ulishuhudiwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Jimbo la Rombo, Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rombo, na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Rombo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rombo, pamoja na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya Dodoma na Rombo mkoani Kilimanjaro.
0 Comments