Header Ads Widget

ADHA YA KUKOSA HUDUMA ZA AFYA YATOWEKA KWA WAKAZI WA IVILIKINGE MAKETE NJOMBE

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wananchi kutoka Kijiji cha Ivilikinge  wilayani Makete mkoani Njombe, wameondokana na changamto za kufuata huduma za afya umbali mrefu baada ya wadau wa maendeleo kufanikisha kujenga zahanati na kisha kukabidhi vifaa tiba, vikiwemo vitanda vya kujifungulia na uchunguzi wa magonjwa kwa binadamu ili kunusuru vifo visitokee.


Wananchi wa Kijiji cha Ivilikinge Kata ya Isapulano  Wilayani Humo Beiya Tweve na Ascioli Tweve wameonesha furaha yao baada ya Zahanati yao kukamilika na Wadau wakiwemo Benki ya NMB Kusaidia baadhi ya Vifaa vya Kutolea huduma za Afya.



Wakazi hao wameshuhudia vifaa tiba vikikabidhiwa rasmi kuanza kuwahudumia  baada ya Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kutoa vifaa hivyo kupitia  asilimia moja kila mwaka ya faida inayopatikana kurudishwa kwenye jamii.



Willy Mponzi ni Kaimu meneja wa Benki ya NMB Kanda ya nyanda za Juu Kusini ambaye anasema mbali na kutoa vitanda viwili vya kujifungulia na vitanda viwili vya uchungui lakini miaka miwili iliyopita walishatoa bati 200 wakati wa ujenzi.


Akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Ivilikinge katika hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba iliyohudhuriwa na mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana ambaye pia ni mbunge wa Viti maalum mkoa wa Njombe,Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo  Hassan Yusuph amesema nguvu za wananchi katika ujenzi huo zimetumika zaidi ya shilingi milioni 26.5.



Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya ili taifa liendelee kupata nguvu kazi ya kusukuma maendeleo.


Kujengwa kwa Zahanati hiyo na kupatikana kwa vifaa hivyo kumerejesha sura za furaha kwa wakazi wa Ivilikinge ambao wametaabika kwa miaka mingi katika kutafuta huduma za afya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI