Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WATANGAZA RASMI HAKI WANAZOPIGANIA

 

Na MWANDISHI WETU


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Act Wazalandio Taifa Omar Ali Shehe ametangaza rasmi haki za msingi wanazozipigania chama hicho ikiwemo Wananchi kupata huduma bora na kila mwananchi kupata haki ya kikatiba ya kuishi.



Naibu Katibu Mkuu huyo alisema hayo wakati akihutubia Wananchama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara  uliofanyika katika kiwanja Jongomeo Chambani,Wilaya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.


“Tunapigania haki ya kuchagua viongozi wanaotuongoza  wakiwemo madiwani,wawakilishi, wabunge na  Rais,tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi wazanzibar tunateseka na kuongozwa na watu tuisowataka kuanzia majimbo hadi serikali,”


Alisema Wazanzibar pia wanaoigania haki ya kuwa na Zanzibar yenye mamlaka kamili yenye kiti chake umoja wa mataifa na uwezo wa kujiamulia mambo yake yenyewe ikiwemo uchumi na hakuna chama chingine chenye uwezo wa kupigania mamlaka kamili isipokuwa Act Wazalendo.

Aidha alisema kuna vitendo vimeanza kufanyika vinavyokwenda kinyume na msingi ya Demokrasia baada ya viongozi wa mitaa (masheha) kudaiwa na wananchi wamekuwa wakipita katika nyumba na kuchukua namba za vitambulisho vya mzanzibar Mkaazi au za kadi za wapiga kura bila ya kueleza malengo yake.


“Tumeshuhudia vitendo vinavyoendekea katika mkoa huu wa Mkoani masheha wanapita kila  nyumba na kuchukua namba za vitambulisho vya wapiga kura wakati Serikali inapokuwa na jambo lazima itoe tangazo rasmi kitendo hicho kinachofanywa na masheha hakina nia njema”



Hata hivyo amewataka Wananchama wa chama hicho wasitoe mashirikiano na masheha na badala yake wakaripoti katika matawi ya chama chao ili viongozi wa chama waanze kuchukua hatua za kuwashughulikia masheha wanaofanya vitendo hivyo.


Nae Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Othman Masoud Othman amesema Mapinduzi ya Mwaka 1964 hayakufuta Mamlaka kamili ya Zanzibar ya kuwa na kiti cha dola Umoja wa Mataifa na badala yake yaliweka utaratibu mpya wa uwendeshaji wa Serikali.


Alisema baada ya Mapinduzi kufanyika Sultani aliondoka lakini Zanzibar ilendelea kutambulika kama nchi na uwakilishi katika baraza la umoja wa mataifa kabla ya kuzaliwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar 1964.


“Mapinduzi yalipokuja hayakuja kupindua dola ya Zanzibar yalikuwa yalikuja kubadilisha mfumo wa kuendesha dola ya Zanzibar na ndio maaana kiti chake umoja wa mataifa kilibaki kilekile Umoja wa Mataifa,”


Aidha alisema kwa Wananchi wa Chambani ni alama kubwa inayohitaji kuenziwa kwa sababu Mzanzibar wa kwanza alie ratibu na kusimamia suala la Zanzibar kuwa Mwanachama wa umoja wa mataifa ni Waziri Mkuu wa kwanza baada ya mapinduzi Mohammed Shamte ambae alikuwa mzaliwa wa chamabani Mkoa wa Kusini Pemba.


“Kama kungekuwa tupo katika nchi ambayo inahifadhi historia yake na kuthamini chambani tungejenga mnara wa kumbukumbu wa kuenzi wana chambani, alichokifanya ni alama kubwa ya kwenda kusimamisha Zanzibar kama dola katika Mamlaka ya kimataifa,”


Nae Mjumbe wa Kamati kuu ya chama hicho Seif Khamis amesema wakati vijana wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira walimua kujiajiri kuanzisha biashara ndogondogo bahati mbaya walikuwa wanapata usumbufu mkubwa wa kufukuzwa katika maeneo ya biashara na mabaraza ya miji kisiwani Pemba 


kujengwa masoko mapya bila ya kushirikishwa Wananchi kumechangia masoko mengi kukamilika lakini hayatumiki na Wafanyabiashara  baada ya kujengwa Nje ya mji.


Alisema Wafanyabiashara wanagoma kuhamia katika masoko mapya yaliyojengwa kwa sababu yalijengwa nje ya miji na kuwapa wakati mgumu watu wanaotafuta mahitaji na wafanyabira wenyewe wakiwemo wajasiriamali.


Viongozi wa chama cha Act Zanzibar wamepiga kambi kisiwani Pemba wakitumia muda mwingi kutoa elimu ya masuala ya demokrasia na msingi ya haki za binadamu na utawala bora huku wakonesha kidole Serikali ya Awamu ya nane kuwepo kwa ufisadi katika baadhi ya miradi hasa ya ujenzi visiwani humo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI