Header Ads Widget

4R ZA RAIS SAMIA ZALETA MAENDELEO MAKUBWA ,TUZIHESHIMU ILI ZIKUZE UZALENDO KWA VIZAZI VIJAVYO -MLAWA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.

Mdau wa maendeleo wilayani Kilolo mkoani Iringa Aidan Mlawa akiwa kwenye uhamasishaji maendeleo na amani kata ya Image wilaya ya Kilolo .

Na Matukio Daima App:

Aidan Mlawa ni mdau wa maendeleo wilayani Kilolo mkoani Iringa alijitosa kuonesha uzalendo wa wazi kwa Taifa kwa kuunga mkono 4R za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan .

4R za Rais Dkt Samia  zimeanza wakufikia vema watanzania na wengi Wao wameanza kuziganyia kazi kwa vitendo huku wachache wakitaka kuzitumia kama njia ya kutaka kupenyeza agenda yao ya kutaka kuvuruga amani Nchini .

Mlawa ambae ni mtoto wa mkuluma aliyepata elimu yake kwa shida kwa mama yake mzazi kumsomesha kwa pipa la pombe amekuwa mzalendo wa kweli wa kuenzi Amani kupitia 4R za Rais Dkt Samia.

Anasema kuwa ni wazi tangu Rais Dkt Samia ameingia madarakani Machi 19, 2021 Rais Samia amekuwa na falsafa yake ya R nne (4R) anazozitumia katika utawala wake. 

"4R maana yake ni maridhiano (Reconciliation), mabadiliko (Reforms), ustahimilivu (Resilience) na kujenga upya (Rebuilding)"

Kuwa haya  ndio yatakayoendelea kujenga amani na utulivu wa kudumu nchini kwetu na kuleta maendeleo endelevu, ni hivi sasa  tuna ona fahari nchi imefika uchumi wa kati ngazi ya chini na kuna dalili za kuimarika ili kufikia uchumi wa ngazi ya juu zaidi.

Mlawa anasema anaziona faida kubwa za  4R za Rais Samia katika Maendeleo na Siasa Zenye Tija .

Katika historia ya Tanzania, uongozi umeonyesha mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa. 

Kuwa moja ya mifumo ambayo imeleta mapinduzi ya kipekee ni mpango wa 4R ulioanzishwa na Rais Samia . 

Anasema mpango huu umekuwa nguzo muhimu katika kuinua uchumi wa nchi, kuboresha maisha ya wananchi, na kusimamia mabadiliko katika siasa za Tanzania.

Anasema mpango wa 4R unasisitiza umuhimu wa utawala bora, uwazi, na uwajibikaji. 

Rais Samia ameweka wazi kuwa, ili kuleta maendeleo ya kweli, ni lazima kuwepo na uwazi katika matumizi ya rasilimali za umma. 

Ni ukweli kuwa kupitia mpango huu, serikali imeimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha za umma, ambayo imepunguza mianya ya rushwa na ubadhirifu .

Hata hivyo Mlawa anasema  kwa mfano, ripoti za ukaguzi wa fedha za serikali zimekuwa za wazi zaidi, na hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya watendaji wasio waadilifu.

"Hii imeongeza imani ya wananchi kwa serikali na kuhamasisha ushiriki wao katika miradi ya maendeleo katika wilaya ya Kilolo, Iringa, kumekuwa na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa, kama vile ujenzi wa barabara, shule, na zahanati, Hospitali kubwa ya wilaya yote hii ni  kutokana na uwazi huu wa matumizi ya fedha za umma.

"Rais Samia ameweka mkazo mkubwa kwenye uchumi, hasa baada ya changamoto za janga la UVIKO-19 kwa kupitia mpango wa 4R, serikali imefanya jitihada kubwa kuimarisha sekta mbalimbali za uchumi kama vile kilimo, biashara, na viwanda"

Anasema kuwa hivyo 4R imeleta mafanikio katika kukuza pato la taifa na kuongeza ajira.

Aidan Mlawa, akiwa mdau wa maendeleo katika wilaya ya Kilolo, anasema kuwa kilimo kimeboreshwa kupitia mpango wa 4R, ambapo wakulima wadogo wamepata mbegu bora, pembejeo, na mafunzo ya kilimo cha kisasa. 

Pia, serikali imewekeza katika ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mazao na masoko ya ndani na nje, hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na kupunguza umasikini vijijini.

Mpango wa 4R umechangia katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu muhimu nchini. 

Hii inajumuisha barabara, madaraja, shule, hospitali, na miradi ya maji safi Katika Kilolo mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla .

 Mlawa anaeleza kuwa, barabara ambazo awali zilikuwa hazipitiki, sasa zimeboreshwa na zinaendelea kuboreshwa kwa Kuwekwa lami na hivyo kufungua milango ya biashara kati ya Kilolo na miji mingine kama Iringa na Dar es Salaam.

Pia, kupitia 4R, miradi ya maji safi imewekwa katika maeneo ya vijijini ambapo hapo awali ilikuwa ni changamoto kubwa kwa wakazi kupata maji ya kutosha na safi kuwa kupitia mamlaka za maji Vijijini na mijini kama RUWASA na IRUWASA kazi inaonekana . 

Kuwa Uboreshaji wa miundombinu umechochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za msingi na kupunguza gharama za usafirishaji wa mazao na bidhaa

Kuwa Rais Dr Samia ameonyesha uongozi wa kipekee katika kuleta siasa zenye tija na mshikamano.


 Kupitia mpango wa 4R, serikali imeweka mazingira bora ya demokrasia kwa kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kutoa nafasi kwa vyama vya siasa kushiriki kwenye majadiliano ya kisiasa.

 Aidha, amejitahidi kuleta usawa wa kijinsia katika uongozi, ambapo idadi ya wanawake katika nafasi za maamuzi imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Katika wilaya ya  Kilolo  Mlawa anaona kwamba siasa za mpasuko zimepungua na jamii imekuwa na mshikamano zaidi.

Kuwa  Serikali imekuwa ikitoa elimu ya uraia kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ushirikiano kati ya vyama vya siasa ili kuepusha migogoro ya kisiasa isiyo na tija.

Mpango wa 4R pia umeleta mabadiliko makubwa katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. 

Hata Rais Dkt Samia amefanya jitihada kubwa kuvutia wawekezaji kwa kuboresha mazingira ya biashara, kupunguza urasimu, na kuimarisha sheria zinazolinda wawekezaji.

Anasema kuwa hii imewezesha ujenzi wa viwanda vipya na kuleta teknolojia za kisasa ambazo zimeongeza uzalishaji na ajira nchini.

Mlawa anaona kwamba wawekezaji kutoka nje wameanza kujitokeza, hasa katika sekta za kilimo na madini na Kilolo sasa viwanda zaidi vinajengwa  ambapo teknolojia za kisasa zinaanza kutumika, hivyo kuongeza tija na faida kwa wananchi wa eneo hilo.

 Aidha alisema kuhusu ushirikiano  wa kimataifa umeongeza fursa za kibiashara na kuinua uchumi wa wananchi wa kawaida ni kubwa na hii ni matunda ya ziara za Rais Dkt Samia nje ya nchi .

Hivyo anasema kuwa mpango wa 4R wa Rais Samia Suluhu Hassan ni chombo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa nchini Tanzania. 

Aidha  Mlawa anasema kuwa kupitia mpango huu, serikali imeweza kuimarisha utawala bora, kukuza uchumi, kuboresha miundombinu, na kuleta siasa za mshikamano na tija zaidi .

Kuwa kupitia 4R za Rais Dkt Samia nchini imepata maendeleo na itaendelea kupata maendeleo zaidi kama Kila mmoja ataheshimu na kutumia kwa misingi ya kimaendeleo na ni tunu kubwa kwa Vizazi vijavyo kuona Taifa lenye misingi bora zaidi.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI