Na WILLIUM PAUL, SIHA.
MBUNGE wa Viti Maalum Kundi la Watu Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ametoa zaidi ya shilingi bilioni 43 katika Wilaya ya Siha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo .
Nderiananga aliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Ndumeti, Kata ya Makiwaru iliyopo wilaya ya Siha ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani Kilimanjaro ambapo awali alikutana na kufanya mkutano wa ndani na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Wilaya hiyo.
Alieleza kuwa ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za maendeleo shilingi Bilioni 829 katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
0 Comments