NA WILLIAM PAUL, MWANGA.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angella Kairuki amewahakikisha wananchi wa kata ya Kwakoa wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambao wanadai kifuta jasho cha milioni 165 kwa wale waliothiriwa na Wanyama pori kuwa watalipwa fedha hizo.
Waziri Kairuki alitoa kauli hiyo jana kwa njia ya simu alipompigia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga alipofanya ziara katika kata hiyo kuzungumza na Wananchi.
Kairuki alisema kuwa, wanatambua changamoto wanayokabiliana nayo Wananchi wa Kata ya Kwakoa ya uharibifu na wanyama pori ambapo wanadai kifuta machozi cha milioni 165 na serikali imeshaanza kulipa fedha hizo.
Aidha amewataka Wananchi hao kuzingatia mafunzo yanayotolewa ya kukabiliana na wanyama pori huku akiahidi Wizara yake kupeleka mabomu baridi ya kufukuzia wanyama pori 500 katika wilaya ya Mwanga pamoja na kujadiliana na halmashauri kuona umuhimu wa kununua mabomu mengine ili yapatikane katika kila kijiji.
0 Comments