Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi Mkoani Lindi Juma Mnwele amewahimiza Walimu wa manispaa hiyo kujenga tabia ya kujiwekea akiba ya kiasi cha pesa wanazozipata pamoja na kupangilia vzuri matumizi yao ili waweze kufanya mambo ya kimaendeleo .
Mnwele ametoa Rai hiyo alipokuwa anazungumza na walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka halmashauri ya manispaa ya Lindi na Mtama Katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Benk ya NMB.
Amesema ili waweze kuwa na Maendeleo swala la nidhamu ya pesa ni jambo la kipaumbele hivyo ni muhimu kutumia Mafunzo waliyoyapata Katika kupanua uwezo wao wa kiuchumi sambamba na kupanga maisha Yao.
Faraja Ngongo ni meneja wa NMB kanda ya Kusini Amesema Program hiyo ya mwalimu spesho imelenga Kutoa Masuluishi mbalimbali ya kibenki na utunzaji wa fedha pamoja na kuongeza fursa kwa Walimu ambao wamekuwa ni Wadau wao wakubwa.
Baadhi ya Walimu walioshiliki Katika warsha hiyo wakaeleza manufaa wanayoyapata kutokana na kifurushi hiko.
0 Comments