Header Ads Widget

WATAALAMU WA UJENZI WAPEWA NENO KUKABILI MAJANGA

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma



Katika kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema itaendelea kuweka mikakati na kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya kukabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza ili kupunguza athari zake kwa wananchi.



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Salum Manyata alipozungumza kwenye Semina ya kujenga uelewa kuhusu upunguzaji wa madhara ya maafa katika Jamii, iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ikiwahusisha wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji pamoja na wataalam kutoka halmashauri hiyo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.




Alisema mafunzo hayo yamelenga kundi hilo kutokana na kuwa karibu na jamii ambayo inaguswa moja kwa moja yanapotokea maafa hivyo ujuzi wanaoupata utaisaidia jamii katika maeneo wanayoishi kupunguza athari na kuongeza uelewa na uwezo wa kuchukua tahadhari.


Kwa Upande wake Mshiriki wa semina hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bugamba Kata ya Mwamgongo Wilayani Kigoma Moshi Ahmadi amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kutambua viashiria na hatua wanazotakiwa kuchukua kabla, wakati na baada ya kutokea kwa maafa.



"Naishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutuwezesha kupata ujuzi huu kupitia semina hii kwani majanga yamekuwa yakitokea katika maeneo yetu na tukawa hatujui hatua sahihi za kuchukua lakini kwa sasa tumeweza kufahamu nafasi na majukumu yetu ya kukabiliana na maafa katika vijiji" amesema menyekiti huyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI