Header Ads Widget

WATAALAMU WA AFYA YA KINYWA NA MENO WAHITAJIKA ZAIDI NJOMBE

Na Gabriel kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Vyuo vya Afya nchini vimetakiwa kuongeza nguvu katika utoaji mafunzo katika masomo ya Afya ya kinywa na meno kutokana na uhaba mkubwa wa wataalamu wa sekta hiyo.


Rai hiyo imetolewa na Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dokta Juma Mfanga akiwa mgeni wa heshima katika mahafali ya 9 ya chuo cha Afya Mgao mjini Njombe ambapo amesema licha ya serikali kujenga Zahanati nyingi,Vituo vya Afya na Hospitali kila Halmashauri  lakini changamoto imekuwa kubwa kwenye upande wa wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno jambo ambalo hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa.

Rais wa serikali ya wanafunzi Geofrey Kaunda katika risala ya Wahitimu hao amesema  Utovu wa nidhamu hasa wizi,Miundombinu mibovu ya barabara wakati wa masika ni miongoni mwa changamoto zinazokikabili chuo hicho hivyo wanaiomba serikali kufanyia kazi.


Baadhi ya wazazi akiwemo Emily Kapinga  wanaomba watoto wao kwenda kuwa waadilifu huko waendako ili wakaitumikie vyema Jamii.

Mkurugenzi wa chuo cha Afya Mgao Dokta Adelitus Mgao amewataka wahitimu  kuwa makini katika mitihani yao ya mwisho ili wafaulu vizuri badala ya kuja kuwa kikwazo kwa wazazi wanaotumia fedha nyingi kuwasomesha.

Ofisa Rasilimali watu na mdahili wa wanafunzi chuoni hapo Deus Kuba Amesema wahitimu wa fani za utabibu,Famasia,Ustawi wa jamii,Kinywa na meno wanakwenda kuitumikia jamii sasa  huku Mkuu wa chuo hicho Francis kayombo akisema serikali imewapa fursa ya kuongeza baadhi ya kozi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI