Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.
VIJANA Mufindi Wametakiwa kuacha kuburuzwa kielimu na Watu wenye fikra mgando, ili wafikie mafanikio kielimu, Kiuchumi na Kimaendeleo .
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Ndg Utoaji Mtendamema Katika Kata ya Mapanda Wilaya Mufindi mkoani Iringa .
Ndg.Mtendamema alisema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kihansi Wilayani Mufindi ambapo alisema wanapaswa kujitambua hatua waliopo na wanakoelekea Kielimu.
" Vijana hasa ninyi ambao mko kwenye ngazi ya Sekondari naamini mnajitambua na mnaelewa jitihada za Serikali kwenye sekta ya Elimu hapa Nchini ." Alisema Mtendamema.
Alisema Vijana ni Taifa la leo na kesho na Taifa linawategemea kwa elimu wanayoipata kupitia raslimali zilizopo zinazotolewa na Serikali kwa kuboresha miundo mbinu ya Elimu .
Wanafunzi hao Wametakiwa kudumisha amani na utulivu vilivyopo Nchini ili kutengeneza Umoja na utulivu uliopo kwa Watanzania Vijijini na Mjini.
Alisema sasa hivi Sekta ya Elimu na miundo mbinu yake imeboreshwa kwa kuwekezwa raslimali zote muhimu majengo, madarasa ya Kisasa na maabara hivyo ni jukumu la Wanafunzi hao kujibidisha kimasomo .
Pamoja na elimu hiyo kutolewa kwa Wanafunzi hao Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Kata ya Mapanda Ndg.Mtendamema aliwataka Wanafunzi hao kujitokeza katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura kwa wale wenye umri wa miaka 18 na wale ambao mwakani watakuwa wametimiza umri huo.
" Wanafunzi kumbukeni mwakani 2025 kutakuwa na Uchaguzi Mkuu hivyo mtakuwa na sifa na haki ya msingi ya kupiga kura na kuchagua Viongozi katika ngazi za kisiasa" Aliongeza kusema .
Vijana pia Wametakiwa kuiunga mkono CCM chini ya Uongozi thabiti wa DKT.Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Alisema jitihada zinazofanywa za kuboresha miundo mbinu ya Elimu Nchini ni sehemu ya maono ya DKT .Samia kuboresha elimu ya Tanzania katika kila nyanja.
0 Comments