Header Ads Widget

WAKULIMA WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI ZA KILIMO







Na Hamida Ramadhan Matumio Daima App Dodoma


WAKULIMA Nchini wametakiwa  kuzingatia kanuni za kilimo hasa kwa kutumia mbegu bora zenye ukizani, kupanda mapema kupanda katika nafasi zilizopendekezwa bila kusahau kupalilia kwa wakati. 


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Alssem Dkt, Emmanuel Monyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika banda lao lililopo kwenye viwanja vya Nanenane Dodoma. 


Amesema mkulima ili aone tija ya kilimo chake ni vyema kuhakikisha anakausha mavuno Mara baada ya kuvuna na Kuhifadhi mahali pasipo na unyevu. 


Akieleza umuhimu wa karanga amesema zao hilo ni zao la Mafuta lakini pia hutumika kama chakula cha binadamu huku mashudu na majani yake kutumika kulisha mifugo. 


" Tanzania ni nchi pili kwa uzalisgaji karanga Afrika baada ya nchi ya Nigeria lakini kwa hapa nchini kwetu zao la karanga hustawi zaidi mikoa ya Mtwara, Dodoma, Shinyanga na Tabora , " Amesema Mkurugenzi huyo. 


Naye Emmaculet Chaula ametaja aina za karanga ambazo ni Naliendela ambayo hukomaa kwa siku 90 Hadi 100 na mkulima akilima kutegemea kupata mavuno ya wastani wa tani 1 kwa hekta. 


Ndachi kukomaa kwa siku 110 na mkulima akilima kupata mavuno wastani wa tani 1.1-2 kwa hekta. 


Amesema Nari nut inastawi katika Ukanda wa chini na Kati na pia hukomaa kwa wastani siku 106 Hadi 110 na inatoa mavuno ya wastni wa tani 1.3 Hadi 2 kwa hekta. 


Maeitaja ingine ni Tanzanut inastawi katika ukanda wa miracle 0 Hadi 1500 kutoka usawa wa habari na inakomaa kwa wastani wa siku

116 na inatoa mavuno ya wastani wa tani 1.5 kwa hekta. 


" Ni muhimu mbegu zipandwe mapema wakati wa mvua za kwanza bila kusahau mkulima kupanga mbegu za karanga kwa nafasi yaent meta 10 Kati ya mea na sentimita 50 Kati ya mistari, " Amesema


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI