Header Ads Widget

MATOKEO YA URAIS TLS


 Matokeo ya Uchaguzi mkuu wa TLS kutangazwa wakati wowote japo upopo wa ushindi kwa wakili Boniface Mwambukusi wakili Sweetbert Nkuba ni mkubwa zaidi kati Yao mmoja anaweza ibuka kidedea japo Matokeo Rasmi Bado kutolewa.


Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wameendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi kwa shauku kubwa, huku sehemu kubwa wakionekana wamesimama kwenye vikundi nje ya ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC).

Kazi ya kuhesabu kura ilianza saa 10.00 jioni leo Ijumaa Agosti 2,2024 na wanachama kuingia ukumbini kwa ajili ya kuendelea na mkutano mkuu uliokuwa ukijadili mambo mbalimbali, ikiwemo taarifa ya fedha.

Rais wa TLS, Harold Sungusia anayemaliza muda wake, amewatangazia wajumbe kuwa bado hawajamaliza kuhesabu kura.

Jumla ya wagombea sita wanawania urais katika uchaguzi huo ambao ni Boniface Mwabukuzi, Ibrahim Bendera, Emmanuel Muga, Revocatus Kuuli, Paul Kaunda na Sweetbert Nkuba.

Uchaguzi huo ulianza saa 12.30 asubuhi katika viwanja hivyo na vituo kadhaa viliwekwa katika viwanja hivyo, huku kukiwa na baadhi ya askari polisi wakisimamia usalama.

Mchana leo, Kamati ya Uchaguzi ya TLS iliongeza saa moja kutokana na karatasi za kupigia kura kuisha na kulazimika kwenda kuchapisha.

Chanzo :Mwananchi na vyanzo vingine 

MATOKEO.

YATAKUJIA HAPA


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI