Na Fadhili Abdallah, Kigoma
Shirika la reli nchini (TRC) limesema kuwa litaanza kufanya ukarabati mkubwa wa njia ya reli ya zamani kutoka Tabora hadi Kigoma ili kuimarisha usalama wa njia hiyo ya reli na kupunguza ajali.
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema hayo mkoani Kigoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari alipowatembelea majeruhi wa ajali ya treni iliyotokea Agosti 28 mwaka huu na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa kigoma Maweni na hospitali ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Kadogosa alisema kuwa tayari ukarabati mkubwa wa njia ya reli kutoka Dar es Salaam hadi Tabora umeshafanyika na kwa sasa wataanza kuanzia Tabora kuelekea Kigoma baada ya serikali kutoa fedha kwenye bajeti yam waka huu wa fedha huku akieleza kuwa ukarabati wa njia ya Tabora kuelekea Mpanda mkoa Katavi ukiwa unaendelea.
Mkurugenzi huyo wa TRC alisema kuwa sambamba na Tabora hadi Kigoma pia shirika hilo linatarajia kuanza ukarabati mkubwa wa njia ya reli kutoka Tabora kuelekea Mwanza ambao utaenda sambamba na ukarabati wa kuelekea Kigoma.
0 Comments