Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imewaagiza Wahandisi wa Ujenzi kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ya serikali ili kupunguza mapungufu yanayobainika wakati wa ukaguzi.
Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Cassim Ephrem wakati akitoa ripoti ya utendaji kazi ya miezi mitatu kwa vyombo vya habari na kwamba Miradi 23 imefuatiliwa ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 8.7
Katika Miradi hiyo Takukuru wamebaini miradi 9 ilikutwa na mapungufu madogo madogo ikiwa na Thamani ya Shilingi bilioni 3.1 na kuwalazimu kutoa maelekezo ya kufanyia marekebisho.
Kamanda Cassim amesema baadhi ya miradi kesi zake zipo mahakamani jambo ambalo linapaswa kutiliwa mkazo katika usimamizi.
0 Comments