Na Matukio Daima App Dodoma
Shirika la kukuza utawala bora na uwazi Tanzania (IGT) kwa kushirikiana na Shirika la Basis Internaional la Uganda wamewakutanisha wadau wa sekta ya madini ya kimkakati Tanzania na kuzindua jukwaa la kimtandao la kupiga vita rushwa kwenye madini ya kimkakati.
Unzinduzi wa jukwaa hilo ulifanyika jana Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na washiriki mbalimbali toka Serikalini,ashirika yasiyo ya kiserikali, wachimbaji wadogo na wataalamu toka sekta ya madini.
Akifungua mkutano huo wa siku moja Mkurugenzi wa IGT Bwana Edwin Soko alisema kuwa jukwaa hilo linalenga kutoa nafasi kwa wadau kwenye sekta ya madini ya kimkakati kutumia teknolojia kwenye kuripoti taarifa mbalimbali za rushwa kwenye sekta ya madini ya kimkakati.
Soko alibainisha kuwa madini ya kimkakati yana uhitaji mkubwa Duniani hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuzuia biashara haramu ya madini hayo kwa kuwa yanaikosesha mapato serikali.
Soko aliongeza kuwa jukwaa hilo litakuwa na njia mbadala kwenye kutoa taarifa za rushwa kwenye madini ya kimkakati yakiwemo Earth Rare, Nickel, copper na mengineyo, hali hiyo itasaidia Taifa kupata mapato na kuleta maendeleo kwa watanzania.
Kwa uoande wake Mwakilishi toka Taasisi ya Basis International Don Binyima Bwesigye Uganda alieleza kuwa ujio wa mradi huo ni utekelezaji wa azimio la ICGLR ambapo Nchi za maziwa makuu wallikubaliana kwa pamoja kutengeneza mfumo wa pamoja wa kuzuia rushwa kwenye sekta ya madini ya kimkakati.
Bwasigye alieleza nafasi ya Nchi hizo za maziwa makuu kwenye kulinda rasimalimari zake za asili ikiwemo madin ya kimkakati na kuketa maendeleo kwa watu wake.
Pia alieleza kwamba mradi huo unatekelezwa kwenye Nchi nne za Maziwa Makuu Afrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Zambia na DRC Nchini ya Ufadhi wa USAID Afrika
Naye mtaalamu wa ICT toka Basis International Machael Mayaka aliwaeleza washiriki kuwa jukwaa hilo litawapa nafasi ya kuwasiliana katika ngazi ya kitaifa na kikanda na kujua taarifa mbalimbali za madini ya kimkakati.
Naye kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu Bwana Thomas Masanja alieleza nafasi ya tume kwenye kupokea malalamiko yakiwemo ya sekta ya madini na kusema kuwa jukwaa hilo litazidi kuimarisha ushirikiano.
Naye mkurugenzi msaidizi toka ofisi ya mwendesha mashitaka (DPP) Bwana Renatus Mkude alieleza jinsi ofisi yake inavyofanya kazi kwenye kutafuta ushahidi kwa kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua za kufungua mashitaka zikiwemo kesi za madini ya kimkakati
Warsha hiyo ilikuwa ya siku moja na ilifanyika katika ukumbi wa Mamboya kwenye hotel ya Royal Village Jijini Dodoma.
0 Comments