Header Ads Widget

MNEC ASAS -WATIANIA WANAPISHANA KUTOA RAMBI RAMBI MISIBANI


MNEC Salim Abri Asas akikagua ofisi ya CCM kata ya Kising'a 

Na Matukio Daima App 

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM)Taifa Salim Abri Asas ameonya baadhi ya watia nia wa nafasi mbali mbali wilaya ya Iringa Vijijini ambao wamekuwa wakitamani misiba itokee ili kwenda kutoa pole kama njia ya Kampeni .

Kuwa amezunguka wilaya ya Mufindi na Kilolo hajakutana na aina ya siasa za misibani zinazofanywa wilaya ya Iringa Vijijini kwa watia nia kutumia wapambea Wao kuzunguka misibani kutoa pole misibani.

Akizungumza Leo na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo baada ya kuhitimisha ziara yake ya Siku Moja wilaya hiyo alisema si vibaya kwa watia nia hao kushiriki masuala ya kijamii na kutaka ushiriki huo usiwe sasa wakati wanatafuta nafasi za kugombea ila hata baada ya kukosa nafasi hizo kuendelea kushiriki .

Asas alisema aina ya siasa inayofanyika wilaya ya Iringa Vijijini imemshangaza zaidi kwani imefika wakati watia nia wanatamani misiba itokee ili wafike kutoa pole .

"Niliwahi kusikia na kusoma kwenye vyombo vya habari aina ya misiba ambayo imekuwa ikikodi watu wa kuomboleza hii sasa imefika Iringa Vijijini hawa wapambe wa watia nia wanalia kweli misibani Kuliko hata wafiwa"alisema MNEC Asas

Hata hivyo alisema kutia nia si Dhambi ila ni vizuri watia nia kuheshimu kanuni na taratibu za CCM vinginevyo kanuni zitawawajibisha.

 Awali akikagua ofisi ya CCM kata ya Kising'a Jimbo la Ismani MNEC ASAS alipongeza kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa ofisi na kuwa viongozi wanafanya vizuri wasitolewe kwenye Uchaguzi.

Kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wamefanya kazi nzuri ya usimamizi wa Ilani ya CCM kuwa viongozi hao wasiachwe kwenye Uchaguzi wa serikali za Vijijini na Miata na Uchaguzi mkuu mwakani.

 MNEC Asas alisema ujenzi wa ofisi hiyo na nyingine amezijengwa kwa Udhamini wa asilimia 100  kama njia ya kukiwezesha Chama kuwa na ofisi zenye heshima.

Hivyo Asas alisema viongozi wa kuchaguliwa ambao wameweza kutekeleza ilani vizuri kutoachwa kwenye Uchaguzi ujao na kutaka viongozi hao kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi pamoja na kuhakikisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na CCM inapata kura za kutosha Uchaguzi ujao.

Kuhusu ujenzi wa ofisi hiyo kuwa ya kwanza ndani ya mkoa wa Iringa alisema kata ya Kising'a ni kata ambayo yeye ni mwelezaji na ndio sababu ya kuanza ujenzi wa ofisi ya kwanza kwenye kata hiyo na kata nyingine za wilaya ya Iringa Vijijini ambako tayari ofisi zimekamilika na sasa wilaya ya Kilolo,Mufindi na wilaya nyingine wameanza.

Wakati huo huo MNEC Asas ameahidi kukamilisha maboma ya shule ya msingi Kising'a ambayo Bado kukamilika na kuwa ujenzi huo ataukamilisha kabla ya Uchaguzi wa serikali za mitaa kufika ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira Bora zaidi.

Katika ziara yake hiyo wilaya ya Iringa Vijijini MNEC Asas amekabidhi simu zaidi ya 155 Kwa ajili ya kusaidia kusajili wanachama kidigitali 

Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini Rehema Mohamed  alisema kuwa CCM wilaya ya Iringa Vijijini imeendelea kufanya ziara za kujenga Chama na kuwa tayari kwenye ziara hizo imepokea wanachama zaidi ya 100 kutoa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)na Vyama vingine ambao wanavutiwa na utendaji kazi wa CCM .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI