CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA YA KULAANI NA KUPINGA VITENDO VYA JESHI LA POLISI KUZUIA VIJANA WA CHADEMA KUADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI .
Ulimwengu mzima unaadhimisha siku ya vijana Kila tarehe 12 Agosti, ya Kila Mwaka .
Vijana wa Tanzania ambao sio Wana CCM wanazuiliwa na jeshi la Polisi na Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa Sisty Nyahoza kuwa vijana wa Chadema (BAVICHA) wasikusanyike ili kuadhimisha siku hii, kinyume na sheria ! Kwa taarifa za 'ramli' iliyoandaliwa na Msajili Msaidizi wa Vyama kwani barua yake aliyompa nakala Mkuu wa jeshi la Polisi ndio sababu zilizotumiwa na jeshi hilo kuzuia na kukamata vijana maeneo mbalimbali ya nchi wakiwa safarini kuelekea Mbeya kwenye maadhimisho ya siku yao .
Kwa hatua ya Sasa tunasema yafuatayo;
1. Chadema tunalaani vikali na kupinga Kwa nguvu zote ubaguzi huu unafanywa na Msajili Msaidizi wa Vyama akishirikiana na jeshi la Polisi nchini .
2. Tunamtaka Mkuu wa jeshi la Polisi awaachie vijana wote waliokamatwa wakiwa safarini ili waendelee na safari waliyokusudia kwani haijawahi kuwa kosa la kisheria kusafiri kutoka eneo Moja la nchi kwenda eneo lingine. Katiba yetu imetoa uhuru huo Kwa wananchi ,hivyo kuendelea kuwashikilia na kuwakamata ni kuvunja Katiba .
3. Jeshi la Polisi waache mara moja kuwahoji na kuwafungulia majalada ya kesi kubwa za uongo kabisa kama walivyofanya Polisi wa kituo Cha Polisi Mikese -Morogoro ambao wamefungua jalada la 'Usafirishaji haramu wa Binadamu'( Human trafficking) ni kielelezo cha wazi kuwa Polisi hubambikia watu kesi hapa nchini.
4. Rais wa nchi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu kama hajatoa maelekezo Kwa Msajili Msaidizi wa Vyama vya siasa aingilie kati na Vijana wa Chadema waachwe washiriki na Vijana wenzao Ulimwenguni kusherehekea siku Yao kama hatafanya hivyo itakuwa ni wazi kuwa ameamua kuachana na R4 ambazo amekuwa akizisema !
5. Mpaka muda huu (18:00) vijana zaidi ya 281 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika vituo mbalimbali kama ifuatavyo;
i) Temeke Vijana 11
ii)Mbeya Vijana 10
III) Iringa kituo Cha Kati 104
Iv ) Migori Ismani Vijana 35
V) Makambako vijana 74
Vi) Mikese Morogoro Vijana 48
Imetolewa Leo Jumapili tarehe 11 Agosti,2024.
John Mrema - Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
0 Comments