Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.
MGOGOLO Wa nauli kati ya Wananchi wanaotumia usafiri wa Bajaji na Waendesha Bajaji Mafinga Mamlaka zadai hekima inatakiwa ili kuondoa mkanganyiko wa bei kutoka kituo kimoja kwenda kingine.
Kumekuwepo na mgogolo wa abiria kulalamika kupandishiwa nauli za Bajaji katika Halmashauri ya Mji Mafinga mkoani Iringa na kupelekea kero kubwa isiyokuwa na ufumbuzi.
Hivi karibuni Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga waliibua hoja katika kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka 2023/2024 kwa kuomba ufafanuzi kuhusu nauli.
Hoja hiyo ilianza kuibuliwa na Diwani Kata ya Boma Mhe.Jurist Kisoma ambaye alidai Wananchi wanalalamika nauli kupanda kienyeji.
Mh.Kisoma alisema ni muda mrefu abiria wanaamliwa kulipa nauli ambazo Waendesha Bajaji wanataka kwani awali ilikuwa kituo hadi kituo sh.500 kwa daladala na zilipoanza Bajaji wakawa wanazikodisha kwa makubaliano ya Dereva na mteja anakokwenda kulingana na umbali .
Mhe.Kisoma aliliambia Baraza kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida abiria wameanza kulipishwa nauli kati ya sh.800,1000, 3000 hadi 5000 jambo ambalo alisema halikubaliki.
" Mkurugenzi nashukuru na Mhe .Dr.Linda Salekwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi yupo hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi.Fidelica Myovella wapo labda Afisa Biashara Bw.Evance aliambie Baraza nauli hizi zinapangwa na nani?" Alihoji Mhe.Kisoma.
Afisa biashara Halmashauri Bw.Evance Mtikile alisema kwanza mgogolo huo anaufahamu na kwamba suala hilo lipo kwa Afisa mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Iringa kwani wao ndio wapangaji wa nauli na Halmashauri haihusiki.
Bw.Mtikile alisema LATRA wanatarajia kuingia Mafinga august 17 katika Ukumbi wa Halmashauri ya kwa ajili ya kikao kati ya Halmashauri,LATRA na Madereva Bajaji .
August 17 maafisa wa LATRA walifika na kukutana na Waendesha Bajaji, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Regnant Kivinge na Afisa biashara Bw.Evance Mtikile ambapo hitimisho waliachiwa Waendesha Bajaji waone jinsi ya kufanya maana hakuna kipengele kinacho waruhusu LATRA kupanga nauli maana hiyo ni biashara ya kukubaliana kati ya mteja na Dereva wa Bajaji.
Kiongozi wa Chama cha Bajaji Mafinga Bw Harun Manga alisema sababu kubwa ya kupandisha nauli ni gharama za uendeshaji kupanda kwa vipuri na Mafuta na ni utaratibu walioamua kuufuata ili kuweza kukidhi matakwa ya biashara.
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.Regnant Kivinge alisema katika hali ya kawaida Wananchi na abiria katika Mji wa Mafinga na viunga vyake wanateseka sana na hawana msaada tena na hakuna wa kuwatetea.
"Mimi kama Mwenyekiti wa Baraza la madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga siamini kabisa kuwa Bajaji hawana mdhibiti wa mfumko wa bei za nauli ,siamini na katu sitaamini ." Alisema MH.Kivinge.
Meneja Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Iringa Bw.Fredrick Shayo alisema Bajaji wanachokifanya ni kosa hivyo wanatakiwa kufanya busara na hekima kwa kuelewana na Wateja wao ,
"Kifupi Bajaji wanachokifanya cha kupakia abiria kama daladala ni kosa kwani walitakiwa kuwa wanasimama kwenye Vituo vyao halafu Wateja wanakodisha na kinachofanyika sisi LATRA hatuna maamuzi bali hekima ndio inatakiwa kutawala ili abiria wasiumizwe." Alisema Ndugu Shayo.
Hata hivyo baadhi ya Wadau wa usafiri wa Bajaji katika nyakati tofauti walisema Bajaji ni kama wapo juu ya Sheria au ni miradi ya Watu Wakubwa ndio kila mara katika Mkoa wa Iringa wamekuwa ni changamoto na hawachukuliwi hatua.
0 Comments