Header Ads Widget

NAIBU MEYA URIO ATOA CHOZI, AOMBA MSAADA KUMCHANGIA MGONJWA KALUME ALLY

 

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni jiji Dar es Salaam, Michael Urio pamoja na Mkurugenzi wa Upasuaji katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili wakimjulia hali Kalume Ally (41) ambaye amelazwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi, mapema Leo Agosti 27,2024

Naibu Waziri akilia kwa uchungu

Na, MATUKIODAIMA App DAR

NAIBU Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Michael Urio  ameiomba serikali, viongozi na wabunge kujitokeza kwa wingi kuwezesha msaada wa matibabu kwa kijana Kalume Ally (41) ambaye mwili wake una uvimbe usiokuwa wa kawaida na kumsababishia maumivu makali.


Urio ambaye amemtembelea mgonjwa huyo leo Agosti 27, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  amesema Kalume yupo kwenye maumivu makali na kuuomba uongozi wa hospitali kumsadia kwa kumfanyia vipimo haraka ili aweze kupata matibabu na huduma stahiki.


"Nimefika wodini, nimebahatika kumuona ndugu yetu, kwa kweli yupo kwenye maumivu makali sana, ameniambia na nimemuona, ombi langu kwa uongozi wa hospitali ya Muhimbili tumsaidie ndugu yetu huku sisi tukiendelea kuiomba jamii imsaidie kwa hali na mali, naaamini tutafanikiwa" alisema Urio.


Mbali na wabunge, Urio amewaomba mawaziri, madiwani na watu mbalimbali kujitoa kumchagia Kalume msaada wa fedha za matibabu.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa MNH,  Dkt Rachel Mhavile amesema, mgonjwa huyo alipokelewa Agosti 24 mwaka huu akitokea Hospital ya Rufaa Temeke, na tayari ameshachukuliwa vipimo vyote. 


Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Mhavile amesema:


"Tayari mgonjwa hiyo amekwisha kuchukuliwa vipimo vyote na tunangoja majibu ya vipimo hivyo ili tuone tunaanzia wapi. Kwa Sasa anapewa dawa za kutuliza maumivu," amesema  Dkt. Mhavile.


Mgonjwa huyo aliibuliwa na  Klabu ya waandishi wa habari wa Dar es Salaam (DCPC) kupitia kwa mmoja wa wanachama wake, Kalunde Said.


Baadaye waandishi kwa umoja wao waliamua kuchangishana fedha hadi kuwezesha kumfikisha mgonjwa huyo Hospitali ya Rufaa Temeke kabla ya kupelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. 


Mwakilishi wa Kamati ya kuratibu matibabu ya mgonjwa huyo kutoka DCPC, Careen Mgonja, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ukarimu waliouonyesha kwa mgonjwa huyo huku   huku akiomba wadau na Watanzania wengine kuendelea kuchangia kupitia namba maalum ya aliyeteuliwa kusimamia matibabu hayo.


"Watu wote watakaoguswa kusaidia kuchangia mgonjwa wanaweza kutupatia kiasi chochote cha pesa kupitia kwa Mratibu Mkuu wa zoezi hili Bi. Kalunde Saidi kupitia namba ya Airtel 

0684695698. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI