Header Ads Widget

MNEC ASAS:TUANZE SASA KUTAFUTA USHINDI WA KISHINDO WA DKT SAMIA 2025

MNEC Salim Abri Asas akikabidhi msaada wa simu janja  155  katibu wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini Rehema Mohamed Kwa ajili ya kusaidia kusajili wanachama kidigitali 

Na Matukio Daima App 

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya chama Cha mapinduzi Taifa (NEC) Salim Abri Asas amewataka wanachama wa Chama hicho na viongozi kuelekeza nguvu katika Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu ili matokeo ya Uchaguzi huo yawe dira ya ushindi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na CCM mwakani 2025.

Alisema kuwa pamoja na pilikapilika za watia nia zilizopo Kwa sasa majimboni na kwenye kata ni vema Kwa sasa pilikapilika hizo zikasitishwa ili nguvu Zote kuelekezwa kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa .

Kuwa hakuna faida ya Wana CCM kuendelea na pilika pilika za Uchaguzi mkuu wa mwakani 2025 wakati hakuna mwenye majibu ya Uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo ni lazima kutumia nguvu zaidi kushinda Uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utatumika daraja la Uchaguzi mkuu mwakani.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake ya kuimarisha Chama katika wilaya za Mufindi ,Kilolo na Iringa Vijijini MNEC Asas alisema hadi sasa uhai wa CCM ni mzuri ila shauku ya Chama kuona uhai huo unaendelea kuwa mzuri zaidi .

Kwani alisema hata baadhi ya watia nia wanaojipitisha maeneo mbali mbali kushawishi muda ukifika kuchaguliwa ni sawa ila wanakiuka kanuni za kuteuliwa za CCM kuwa hata kama wanamisaada inayotakiwa kutolewa kwa jamii CCM inautaratibu wake wa kupokea misaada hiyo na kufikisha sehemu husika ila sio mtia nia mwenyewe kupeleka misaada bila hata Chama kujua.

"Niwaombe sana Wana CCM wote kuheshimu kanuni za Chama wasioheshimu kanuni watawajibishwa kufyekwa na kanuni hiyo".

MNEC Asas aliwataka watia nia wote kusitisha pilikapilika majimboni kwa sasa ni kufanya kazi Moja ya kujenga Chama na kuwaeleza wananchi mazuri ya CCM ili waendelee Kuchangua Chama Daima .

"Niwaombe watia nia wote Kwa sasa simameni pilika pilika zenu acheni Chama kifanye kazi ya kutafuta ushindi wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kitendo Cha watia nia kuendelea na Vurugu zao wanachafua Chama "alisema Asas..

Kuhusu kazi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alisema kazi zake nzuri zimekiheshimisha Chama kuendelea kuaminika zaidi .

Hivyo ni wajibu wa Wana CCM wote kuendelea kuzinadi kazi hizo kwa wananchi .


Akiwa wilaya ya Iringa Vijijini MNEC Asas alipongeza heshima kubwa aliyopewa ya kuvishwa Mavazi ya kimira mfano ya Chifu Mkwawa pia kupewa zawadi nyingi mbali mbali .

"Naomba nianze kwa kushukuru heshima kubwa mlionipa nikiwa Kilolo nilisema zawadi walizonipa sikuwahi kupokea toka nimekuwa MNEC ila hapa Ninyi mmevunja Rekodi zawadi mlizonipa sijawahi pata toka nizaliwe" 

Kwa upande Wao wanachama wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya Iringa ,Kilolo na Mufindi Wamepongeza ziara hiyo ya MNEC Asas kuwa imekiheshimisha Chama .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini Sitivin Mhapa alisema ziara hiyo imechagiza mazuri ambayo serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya na kuwa kupitia ziara hiyo wajumbe wa Halmashauri kuu za CCM wilaya hiyo wamepata elimu nzuri.

Huku Josephat Mwagala mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mufindi akipongeza ziara hiyo kuwa imekuwa na elimu zaidi kwa wanachama .

Said Kiponza mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kilolo alisema Siku Zote kanuni za CCM zipo ila sio wote wanasoma kanuni hizo na kuwa kupitia ziara ya MNEC Asas wengi watakwenda kusoma kanuni hizo.

Wakati katibu wa CCM wilaya ya Kilolo Christina Kibiki na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini Costantino Kiwele wakipongeza jinsi ambavyo ziara ya MNEC Asas ilivyoacha neema katika wilaya zao kwa kupewa simu zaidi ya 100 Kila wilaya Kwa ajili ya kusajili wanachama kidigitali pia ukaguzi wa ujenzi wa ofisi za kata kwenye wilaya Zote.

Ziara ya MNEC Asas ndani ya mkoa wa Iringa imepangwa kuhitimisha Jumamosi Augosti 10 katika Wilaya ya Iringa mjini .

MWISHO 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI