Header Ads Widget

MASHABIKI WA SIMBA MAKIBA WAFANYA USAFI KITUO CHA AFYA CHA MAKIBA


NA RAYMOMD MINJA ARUSHA

Kuelekea Kilele Cha Simba Day Leo 03/08/2024 Mashabiki Wa Simba Wa Makiba mwilaya ya Arumeru mkoano Arusha leo Wamefanya Usafi Kwenye Kituo Cha Afya Makiba .

Akizungumza mara baada ya kufanya usafi mwenyekiti wa tawi la simba Bakari Mambea alisema kuwa lengo la kufanya usafi kwenye kituo hicho ni katika kuadhimisha siku ya Simba day

Mambea alisema kuwa waanachama wa tawi hilo wameamua kufanya usafi na jambo hilo halitakuwa mara ya mwisho bali litakuwa ni la muendelezo kila inapofika siku ya Simba day

Naye katibu wa tawi hilo Kisaka Elieza alisema kuwa wanachama wa tawi hilo wanampango wa kufungua ofisi na tawi

"Kutokana na mwitikio mkubwa wa wanachama tunampango wa kufungua tawi kubwa katika eneo letu na tunategemea kiongozi mkubwa kuja kuzindua tawi hili kwa ajili ya wakereketwa na mashabiki wa tawi hilo"

Kaimu Mganga mfawidhi Kituo Cha Afya Makiba Dr Yusuph Kifumgo Aliwashukuru na Kuwapongeza mashabiki wa Simba kwa kufanya usafi kwenye kituo hicho huki akiwata Kuwataka kuendelea na moyo huo kufanya shughuli za kijamii .

" Ndugu zangu wana simba niwashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri mliyofanya siku ya leo kufanya usafi kwenye kituo chetu cha makiba tunawashukuru sana hili ni jambo zuri na la kuigwa hivyo tuwaombe na wadau wengine kuiga mfano wenu kwa kufanya shughuli za kijamii kama mlivyofanya ninyi hii leo asanteni sana." alisema dr Kifungo

Dr alisema kuwa jambo lililofanywa na mashabi wa simba ni jambo zuri na la mfano na kuaataka mashabiki wa timu nyingine kujitokeza kufanya shuguli mbalimbali za kijamii ka zilivyofanywa na wamashaniki kindaki ndaki wa timu ya simba

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI