ABC UPPER CLASS LTD -ya tatu.
Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP.
MAKAMPUNI MATATU YA MABASI NCHINI YAMEPATA TUZO NA VYETI Kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA imetoa tuzo na Vyeti vya pongezi kwa Wasafirishaji Wakubwa wenye Mabasi zaidi ya 30 .
Akikabidhi tuzo na Vyeti vya pongezi kwa Wasafirishaji Wakubwa waliopata tuzo na Vyeti hivyo Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mhe.Daniel Barani Sillo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mhe.Sillo alikabidhi tuzo na Vyeti vya pongezi katika makampuni hayo kwa niaba ya Mhe.Dkt Phillip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Picha namba 1 tuzo na Vyeti vya pongezi.
Kampuni ya kwanza kupata tuzo na Vyeti vya pongezi ni SHABIBY LINE ya pili ikiwa ni HAPPY NATION CO.LTD na kampuni ya tatu ni ABC UPPER CLASS .
"Napenda kuwakaribisha katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani mwaka huu 2024 yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kuanzia tarehe 26/08/2024 hadi tarehe 31/08/2024."Alisema Mhe.Sillo.
Upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya kutetea haki za abiria (TAKUHA) Bw.Hassan Mchanjama ameipongeza LATRA kwa kuthamini na kutambua juhudi na Uwajibikaji wa Makampuni hayo katika kutoa huduma nzuri na zenye kukidhi matakwa ya biashara za kusafirisha abiria.
Bw.Mchanjama alisema TAKUHA inayapongeza makampuni hayo na kuomba makampuni mengine kupambania tuzo hizo ili kuongeza huduma katika maeneo mbali mbali ya Tanzania .
"Sisi TAKUHA tunatoa pongezi kwa Mamlaka zote hapa Nchini kwa kushirikiana vyema na Wasafirishaji pamoja na Wadau katika kusukuma mbele gurudumu la Sekta ya usafirishaji hapa Nchini". Alisema Bw.Mchanjama.
Aidha Meneja wa kampuni ya Mabasi ya ABC UPPER CLASS LTD katika stendi ya Mabasi Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa alitoa shukurani kwa LATRA kwa kutoa tuzo na Vyeti kwa Washindi.
" Tunawashukuru Wadau mbali mbali na Mamlaka za Serikali kwa Ushirikiano wanao utoa bila kuwa sahau Wadau wetu Wakubwa wa TAKUHA Nchini ". Alisema Kaguo.
MWISHO
HIVI WAJUA APP YA MATUKIO DAIMA INAKUPA HABARI ZOTE KWA WAKATI KARIBU KUJITANGAZA KUPITIA APP HII AMA KUPITIA CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV KWA MAWASILIANO PIGA SIMU 0754026299
0 Comments