Vyombo vya habari na wanahabari nchini wametakiwa kuwa sehemu ya utoaji na uelimishaji sahihi wa zoezi la Uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani .
Kuwa sheria za Uchaguzi zimekuja na maelekezo mbali mbali ambayo wananchi Wanapaswa kujua.
" Ukisoma Kifungu 156 kinaeleza wazi kuwa Kasoro ya jina au maelezo yasiyo sahihi ya mtu yeyote au sehemu iliyotajwa au kuelezwa katika Daftari, taarifa, au nyaraka nyingine zilizotayarishwa au kutolewa chini ya Sheria hii, haitaathiri kwa namna yoyote matumizi ya Sheria hii kuhusu mtu huyo au sehemu hiyo, endapo mtu huyo au sehemu hiyo itaweza kutambulika katika Daftari, taarifa, au nyaraka husika"
Akitoa Mafunzo Leo jijini Dodoma kwa waandishi wa Habari nchini juu ya uandishi wa habari za Uchaguzi mkufunzi Deus Kibamba alisema vyombo vya habari vinawajibu wa kuendelea kutoa elimu Bora na sahihi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusoma sheria za Uchaguzi .
0 Comments