Header Ads Widget

HAMAD MASOUD HAMAD ACHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA PROF.LIPUMBA

 


Na Thabit Madai, Zanzibar 

thabitmadai5@gmail.com 


KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Hamad Masoud Hamad   leo Ijumaa Agosti 23,2023 rasmi anachukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti  wa chama hicho Taifa.


Uchaguzi wa chama cha Wanachi CUF unatarajiwa kufanyika Septemba 14 hadi 15 ambapo nafasi mbalimbali  ndani ya chama hicho zinatarajiwa kugombewa.


Kwa sasa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ni Prof. Ibrahim Lipumba ambae anatarajiwa kujiuzulu nafasi hiyo katika mkutano mkuu.


Zoezi la kukabidhiwa Fomu ya kuwanja nafasi hiyo amekabidhiwa na na Mwenyekiti wa Wilaya ya Magharib B Unguja kichama.



Alizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Katibu Mkuu Hamad Masoud Hamadi amesema kuwa tayari amekamilisha tararibu na wajibu wa kanuni na sheria za chama hicho ambapo amechukua fomu katika wilaya ambayo anaishi.



"Taratibu za chama chetu zinaeleza kuwa mgombea atachukua fomu na kurejesha kutoka wilaya ambayo anaishi, " Hamad Masoud Hamad.


"Mimi nimejitokeza kugombea nafasi hii kama Mwanachama wa chama mwengine wa chama hichi," amesema.



"Waandishi wa Habari hakuna mgogoro wowote ndani ya chama Chetu cha CUF tunajua nini tunafanya maana jana nmepokea simu na meneo mengi kwanini nagombea nafasi hii licha ya Mwenyekiti  Taifa Prof. Lipumba kuchukuliwa fomu kuwania nafasi hiyo," ameeleza.


Hata hivyo ameeelza kwamba, Chama Cha Wananchi CUF hakina mgombea maalum na mwanachama yoyote ana wajibu wa kuwania nafasi mbalimbali.



Fomu hiyo inatakiwa kurejeshwa ndani ya Siku Tatu huku ikiambata na  malipo maalum.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI