Header Ads Widget

HALMASHAURI YA BUKOBA YAVUKA MALENGO KATIKA UKUSANYAJI MAPATO MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

 


Na, Shemsa Mussa -Matukio daima App-Kagera.


Halmashauri ya Bukoba yavuka malengo katika Ukusanyaji wa Mapato katika kipindi Cha Mwaka 2023/ 2024 ,hatua hiyo imepelekea Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kupewa zawadi ya shukrani kwa kusimamia vema Miradi ya Maendeleo na Ukusanyaji Bora wa Mapato.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mhe, Murshidi Hashimu Ngeze ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Taifa, baada ya Majadiliano katika Mkutano wa baraza la Madiwa la kufunga mwaka wa fedha 2023/2024 baada ya halmashauri hiyo kuvuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani kwa asilimia 117% ambapo halmashauri ilipanga kukusanya bilioni 41.189 na imevuka malengo kwa kukusanya Shiling Billion 46.521.


Mhe Ngeze amesema kuwa matokeo hayo ni kutokana na juhudi za watumishi wa halmashauri hiyo na mpaka Sasa hakuna miradi iliyokwama, pia amewasihi watumishi wote kudumisha ushirikiano zaidi ili kuepuka kukwamisha shughuli za Serikali kwa ajili ya manufaa ya wananchi,amesema kwa Sasa ni vema kutengeneza mpango mkakati wa kiuchumi kwa kubuni miradi mipya.



" Ndg Waheshimiwa Madiwani wenzangu naona mmelidhia kumpatia zawadi Mkurugenzi Wetu kwa kazi aliyoifanya sawa tumpatia motisha ili fanyanye kazi zaidi yeye atachukua zawadi hii kwa niaba ya wafanyakazi wote hapa, na kazi iliyobaki Sasa ni kubuni miradi mipya ikibidi tujifunze kutoka sehemu mbalimbali ili Halmashauri yetu izidi kupata hati safi na wananchi wapate maendeleo,amasema Mhe Ngeze"


Aidha nao baadhi ya Madiwani waliohudhulia Mkutano huo Sadoth Ijunga kutoka kata Mikoni ,Seveline kijoma kutoka kata kyaitoke,Jasson Lwenkomezi kutoka kata Kaibanja pamoja na Deogratias Kaijage kata Kishogo walipata wasaa wa kutoa maoni yao katika taarifa iliyotolewa na Bi Fatina Hussein Laay Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wamesema sekta ya afya utoaji wa vitambulisho kwa wazee kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu bure imekuwa changamoto kwani asilimia kubwa ya wazee hawajapata vitambulisho hivyo.


Pia Madiwani hao wameongeza kuwa uwekwe utaratibu mzuri wa kuangalia vigezo kwa watu walioondolewa katika mpango wa kuokoa kaya maskini Tasaf kwani jambo hilo limekuwa kikwazo kwa wanufaika kwani waliowengi ni wajane,wagane,wazee na watu wenye ulemavu,pia wameshauri nguvu kubwa ya utendaji ielekezwe katika kutakua changamoto za vyoo katika shule za msingi hasa shule za vijijini,na kukuza sekta ya kilimo kwa kufufua zao la chai na kahawa kwa wingi ili kuleta matokeo Bora katika kilimo.



Akitoa majibu ya maswali kutoka kwa Madiwani Ndg,Julius Shulla ambae alimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amesema mpaka Sasa watu 3872 wameondolewa TASAF kwa kumaliza muda wao na kuanza kujitegemea ili kuweza kuwapatia nafasi watu wengine wenye uhitaji.


Sambamba na hayo nae Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mhe,Erasto Yohana Sima amewasisitizia Waheshimiwa madiwani licha ya kupata hati safi mfurulizo kwa mara ya tano amewata kuhakikisha wanashirikishwa kikamilifu katika fedha za maendeleo za ukamilishwaji wa miradi zinazotolewa na serikali kuu kwani wao ndio wanajua kwa kina changamoto zilizomo kwenye kata zao.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI